VIJIJI 2480 NCHINI VYAWEKWA KWENYE MPANGO KAZI WA MATUMIZI BORA YA ARDHI

Na Joseph Ngilisho-ARUSHA

 SERIKALI imesema imeandaa jumla ya mipango ya matumizi bora ya ardhi 2,480 katika kipindi cha miaka minne, ambapo vijiji 4,679 vimewekwa katika mipango hiyo kati ya vijiji 12,333 nchi nzima.


Hayo yamesemwa leo juni 23,2025 jijini Arusha na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Deogratius Ndejembi wakati wa ufunguzi wa jukwaa la wadau kutoka sekta binafsi na serikali pamoja na wakuu wa wilaya mbalimbali wakijadili mipango ya matumizi bora ya ardhi.




Mhandisi Sanga alimshukuru Rais Samia Suluhusu Hassan kwa kuiongezea fedha Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi, ambapo jumla ya mipango ya matumizi ya ardhi 4,679 imeandaliwa kati ya vijiji 12,333 ambapo kwa sasa vijiji 7,654 vimesalia pasipo kupangwa.




“Hili ni jambo kubwa la kumshukuru Rais Samia kwa utoaji wa fedha kwa tume na kuwezesha vijiji hivyo kuwekwa katika mipango ya matumizi bora ya ardhi na kuwashukuru wadau kutoka sekta binafsi kwa kushirikiana na serikali katika kupanga matumizi bora ya ardhi,” amesema.

Post a Comment

0 Comments