Na Joseph Ngilisho ARUSHA
MNYUKANO wa Kisiasa kati ya mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo(CCM) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paulo Makonda umechukua sura Mpya Mara baada ya Gambo kutumia Mkutano wake wa hadhara kumshambulia Makonda akiwataka wananchi waende Dar es Salaam kupata taarifa zake jinsi alivyowaumiza watu wasio na hatia.
"Tumeona kuna mtu anafikiri watu wa Arusha hawana kumbukumbu wanataka kuwadanganya na mimi siko tayari kwa sababu ukweli unatabia ya kuishi na chama changu cha mapinduzi kinasema ,nitasema ukweli daima na uongo kwangu mwiko"
Gambo ameshusha tuhuma hizo nzito leo Mei 11,2025 katika mkutano wake wa hadhara eneo la Soko Kuu jijini Arusha,wakati akihutubia wanachama wa ccm na baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo mkoani Kilimanjaro.
"Kuna mambo mengine sikupenda kuyasema nina uwezo mkubwa sana wa kupuuza ,lakini nimechokonolewa sana na watu lakini kwa sababu nimelazimishwa wacha niseme,kuna mtu mmoja amekuwa akijinadi siku nyingi anasema wakati anaenda kwenye send-off alitumia koti langu mimi mtoto wa muuza uji, akisema eti Gambo ameumiza watu wengi"
"Napenda niwaumize ivi mimi na yeye nani ameumiza watu wengi katika nchi hii,nyinyi mnakujua dar es salaam nendeni mkatafute habari zake kule hata kumsalimia mtaogopa"
Bila kumtaja jina Gambo alimshambulia Makonda na kukanusha taarifa za yeye kuumiza watu ila alidai mtu huyo ndio ameumiza watu na kuwataka watu waende dar es salaam kupata taarifa zake na kudai mikono yake ni misafi na amekuwa akisaidia watu mbalimbali wakiwemo walemavu.
Aidha alidai kuwa miradi mingi iliyoanzisha katika jiji la Arusha imeasisiwa na yeye tangu mwaka 2021 na kuwataka viongozi wengine(bila kumtaja) kuacha kudandia gari likiwa kwenye mwendo.
Akizungumzia mradi wa jengo la Utawala la jiji la Arusha alisema alijenga hoja ya mradi huo akitaka ufafanuzi wa ujenzi wa jengo hilo linalotakiwa kuwa na urefu wa gorofa nane akidai mradi huo umeleta hasara ya kiasi cha sh,bilioni 1.8.
"Jengo la utawala lilitakiwa kuwa na gorofa nane,awamu ya kwanza groundfloo wamelipa bilioni 1.81 ,walipomaliza walitangaza tenda akapatikana mkandarasi wa shilingi bilioni 11.619 na jumla yake ni sh,bilioni 12.7 nikawaambia ukigawanya kwa nane kila orofa litajengwa kwa bilioni 1.587 haikubaliki,haya mambo lazima tuyaseme wawe wamefurahi ama wamechukia "
"Baadaye walisema kwa kuwa sasa hatuna mapato ya kutosha tuingie mkataba mdogo,wakaingia mkataba wa sh,bilioni 6.2 nikapata taarifa na kugundua kwa mkataba huo wameongeza kiasi cha sh,bilioni 1.8 na wakati najenga hoja hiyo walikiri kuleta hasara hiyo "
Wakati Gambo akishusha Nondo hizo,hivi Karibuni RC Makonda alinukuliwa akimrushia makombora ya Mazito Gambo mbele ya naibu waziri mkuu dr Doto Biteko katika viwanja vya Kilombero akimtaka kuwaomba radhi wananchi wa Arusha aliowaumiza akiwa mkuu Mkoa wa Arusha.
Kando na hilo Makonda aliwahi kuwaeleza wananchi jinsi Gambo anavyoishi kwa majungu,fitina na uchonganishi baina ya viongozi na kushindwa kuhudhulia vikao vya Baraza la Madiwani akidai kiongozi wa namna hiyo asiyependa kushirikiana na wenzake ni sawa na mtu anayeishi kishirikina.
Katika Mkutano wa Gambo Leo Madiwani wengi wamegomea kuhudhulia ,kati ya madiwani 32 wa jiji la Arhsha ,waliotambulishwa jukwaani ni wawili tu ambao ni diwani wa Ngarenaro Isaya Doita na diwani mmoja wa viti maalumu na hiyo ni kuashiria kwamba wengi hawamuungi Mkono.
Utafiti mdogo uliofanywa na mwandishi wa Makala haya katika jiji la Arusha unaonesha kwamba Mrisho Gambo anakubalika zaidi na makundi ya akina mama wenye kipato cha chini,huku Makonda akijizolea umaarufu zaidi kwa wananchi wengi ,viongozi mbalimbali ,vijana na wazee ambao aliwasaidia sana matibabu bure pamoja na msaada wa kisheria wa mama Samia legal aid uliowasaidia wengi waliokuwa na changamoto za kunyimwa haki.
Ends.
0 Comments