Na Joseph Ngilisho-ARUSHA
MKE wa mbunge wa jimbo la Arusha mjini ,Magreth Muro ,amesema kuwa Gambo anawajibu wa kutekeleza ahadi alizowaahidi wananchi wa jimbo hilo .
Adha Muro alisema Gambo sio mwanaume boya na kama angekuwa boya asingekubali kuolewa naye na angeshaomba Talaka siku nyingi huku akisisitiza kuwa kaskazini hawaolewi na maboya.
Muro ameyasema hayo leo Mei 10,2025 katika Mkutano wa hadhara wa mbunge huyo, Mrisho Gambo uliofanyika katika viwanja vya Soko Kuu jijini hapa, baada ya kukaribishwa katika jukwaa ,ambapo pamoja na kumwagia sifa nyingi mumewe, ikiwemo kumwita chuma cha pua, aliwaaminisha wanaccm waliokuwa katika mkutano huo kuwa Mumewe sio boya bali ni mchapa kazi .
"Kama Gambo angekuwa Boya nisingekubali kuolewa naye ningeshaomba Talaka,Gambo sio mtu wa blabla ,Gambo sio mtu wa porojo Nyingi kwanza akisikia kelele kichwa huwa kina muuma ,ni mtu anayependa kufanya kazi na akiahidi jambo huwa anafanya"
Ends....
0 Comments