Na Joseph Ngilisho -ARUSHA
BENKI ya CRDB imekabidhi hundi zenye thamani ya sh,milioni 10 kwa washindi kupitia kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda inayosema 'PANDA MITI USIPANDE FITINA' ikiwa na lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti kwa viongozi wa Mitaa ,Vijjji ,vitongoji na Mashina.
Hundi hizo pamoja na tuzo zilikabidhiwa na Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati dkt, Dotto Biteko katika Hafla za sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika Kimkoa katika viwanja vya Kilombero jijini Arusha.
Akiongea baada ya makabidhiano hayo meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini ,Cosmas Sadat alisema benki hiyo imeamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha na kutunza mazingira kwa kutoa kitita cha fedha kwa washindi wa mitaa vijiji na vitongoji watakaokuwa wamefanya vizuri kwa utunzaji wa mazingira na upandahi wa miti.
Alisema benki hiyo imeingia makubalino hayo ikiwa ni mchango wao katika sekta ya Mazingira ili kuhamasisha jamii kushindana kutunza mazingira kwa kupanda miti na washindi watakuwa wakizawadiwa fedha Tasilim.
"Tupo hapa kukabidhi hundi maalumu kwa ajili ya washindi wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira,tumekabidhi hundi mbalimbali za washindi kuanzia sh,milioni 5 , milioni mbili na milioni moja,tunafanya hivi baada ya kupokea ombi la Mkuu wa Mkoa Paulo Makonda na sisi kama benki tuliona ni jambo jema kushiriki kwa njia ya kuchangia fedha ambazo ni sehemu ya faida kidogo tunayopata na kuirejesha kwa jamii"
Awali Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda alisema kuwa zoezi hilo ni endelevu na litakuwa linafanyika kila baada ya miezi mitatu kwa kuzawadia washindi wa mazingira.
Kwa upande wake waziri Biteko aliipongeza benki hiyo ya CRDB pamoja na ubunifu ulioasisiwa na Mkuu wa Mkoa Makonda wa Kuhamasisha upandaji miti kwa kushindanisha mitaa vijiji na mpaka vitongoji lengo likiwa ni kuyaweka mazingira katika hali ya usafi, hongereni sana!
Katika hafla hiyo walionufaika na kampeni hiyo ni pamoja na hospitali ya rufaa ya Mout Meru pamoja na viongozi wa vijiji katika halmashauri ya Arusha DC.
Enda..
0 Comments