BASI LA LIM SAFARI LINALOMILIKIWA NA ELIHAIKA MWANGA LAGONGA NA KUUA MTU MMOJA KATIKATI YA JIJI LA ARUSHA,DEREVA HAKUSIMAMA AKUTWA NA POLISI AKIWA HANA WASIWASI.

 Basi la Lim Safari lagonga na kuua mtu mmoja aliyekuwa pembezoni mwa barabara ,dereva hakusimama hadi stand kuu.

Na Joseph Ngilisho,ARUSHA


Basi la abiria la Kampuni ya Lim Safari linalomilikiwa na Elihaika Mwanga Mkazi wa Mkoani Kilimanjaro,limesababisha kifo cha Mtu mmoja baada ya dereva wa gari hilo kumgonga mtu huyo aliyekuwa pembezoni mwa barabara karibu na stand kuu ya mabasi jijini Arusha.

Tukio hilo linalotazamwa kama ni uzembe wa dereva kwa kutojali wapita njia,limetokea majira ya saa 9 alasiri wakati basi hilo likiingia kituo kikuu cha mabasi jijini hapa.

Dereva wa basi hilo ambaye jina lake
 hakufahamika mara moja, licha ya kutenda tukio hilo hakusimama bali aliendelea na mwendo hadi kituo kikuu cha bus huku akiacha watu wakiduwaa baada ya kujikusanya eneo la tukio huku baadhi wakihoji amepata wapi jeuri hii ya kumgonga mtu na kuondoka.

Hata hivyo baadaye polisi walifika eneo la tukio na kuondoka na mwili wa marehemu ambaye alifahamika kwa jina la ELISANTE NDEOYA anayekadiriwa kuwa na miaka 30 mkazi wa jijini Arusha

Baadaye polisi walifuatilia na kumkamata dereva aliyekuwa akiendesha basi hilo baada ya kumkuta ameegesha  kituo kikuu cha mabasi akiwa hana wasiwasi na kitu alichokifanya 

Picha kwa hisani ya Mtandao.

Ends...

Post a Comment

0 Comments