MSIMAMO WA JIJI LA ARUSHA KUHUSU MADUKA YA WAFANYABIASHARA STAND NDOGO ARUSHA, YADAI WAJENZI HAWANA CHAO NIWAPANGAJI,WALIPE KODI, WAO WACHACHAMAA HATUKUBALI TUMEWEKEZA MAMILIONI

Na Joseph Ngilisho Arusha 

Halmashauri ya jiji la Arusha imewataka wafanyabiashara wanaojiita  wajenzi wa maduka ya biashara eneo la Standi ndogo,kuacha kujidanganya kwani maduka hayo ni mali ya halimashauri nawao wapo hapo kama wapangaji na kuwataka kulipa kodi inayostajili kwa mujibu wa sheria kabla hatua zingine za kisheria hazijachukuliwa.

Akiongea na vyombo vya habari kwa niaba ya mkurugenzi wa jiji hilo,mkuu wa kitengo cha  uhasibu na fedha wa halmashauri hiyo ,Joshua Mwaluko alisema maduka hayo yaliyopo eneo la stand ndogo ni sehemu ya vitega uchumi vya halmashauri hiyo .

Alifafanua kwamba mwaka 2002 halmashauri hiyo ilitoa ridhaa kwa wafanyabiashara kujenga vibanda vya maduka yapatayo 400 kwa makubaliano. 

Alisema hivi karibuni baraza la madiwani liliridhia nyongeza ya kodi kwa wapangaji wa maduka hayo kutoka 200,000 hadi 250,000 jambo linalopingwa na wafanyabiashara wajenzi wakidai kwamba hawawezi kusaini ongezeko hilo la kodi kwa sababu wao ni wamiliki na sio wapangaji hivyo hawawezi kupangiwa kodi bila makubaliano ya pamoja.

"Jambo hili limekuwepo tangia mwaka 2002 ,Ukiangalia mikataba yetu haina mtu anayeitwa mwekezaji mjenzi na muda wa kupata manufaa ya ujenzi uliisha na ndio maana hivi karibuni vyombo vya halmashauri vilikaa na kupendekeza sh, 250,000 kutoka 200,000"

"Eneo yalipojengwa maduka hayo  ni mali ya halmashauri na maduka hayo  yanawapangaji ndio maana kati ya wapangaji 400 wa maduka hayo wapangaji 50 wamesha saini mkataba mpya na kulipa sh 250,000 nao wanaosumbua ni kikundi cha watu wachache"

Awali wafanyabiashara hao kupitia msemaji wao Loken Masawe walisema hawapo tayari kulipa kodi ya sh 250,000 na kuitaka halmashauri hiyo iwape muda wa miezi sita kujadili suala hilo kwa kuwa wao ni wawekezaji wajenzi.

Alisema maduka hayo waliyajenga baada ya makubaliano na halmashauri na sasa ni mali yao na hakuna makubaliano juu ya ukomo wa umiliki na wakiyahitaji wapo tayari kuiuzia halmashauri hiyo kwa gharama za  kipindi hiki.

"Hayo maduka ni mali ya ubia kati yetu wajenzi na Halmashauri ,wao walitoa Ardhi na sisi tukajenga sasa iweje leo wametugeuka na kudai sisi ni wapangaji"

Masawe alisema kuwa suala hilo linahitaji majadiliano ya kina na halmashauri hiyo ndani ya miezi sita ili wafikie mwafaka wa kodi mpya. 

Mkataba wa wajenzi 






Ends...

Post a Comment

0 Comments