MAMA NAIRO ALAMBA UBALOZI MPYA CASSANDRA LINGERIE NI DUKA LINALOBAMBA KWA KUUZA NGUO ZA NDANI 'MWANAMKE ONGEZA MVUTO KWA MUMEO KWA VAZI LA NDANI'

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

                                       

Msanii maarufu wa vichekesho jijini Arusha, Mwangaza Jumanne maarufu kwa jina la MAMA NAIRO  amepata chavu la kuwa balozi wa kutambulisha bidhaa za nguo za ndani za wanawake,kutoka Duka Maarufu la CASSANDRA LINGERIE la Jijini Arusha.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 2, 2023 jijini Arusha, Mkurugenzi wa CASSANDRA LINGERIE, ELIFURAHA MLAKI alisema wanayofuraha kumtambulisha mama NAIRO kama chapa ya sura ya biashara yao kwa lengo la kuleta mapinduzi ya bidhaa zao na  tunaimani anaushawishi mkubwa wa bidhaa zetu kwa wanawake .

“Tunayofuraha kumtambulisha balozi wetu MAMA NAIRO katika safari ya kusimamia brand yetu ya CASSANDRA LINGERIE tunaimani  atahamasisha bidhaa zetu kwa wanawake wenzake  kupitia kazi yake ya uchekeshaji wake katika  jamii"

Alisema wanaimani na MAMA NAIRO kama chapa ya sura ya bidhaa zao na wamejitolea kuwaletea bidhaa bora wanawake kupitia kauli mbiu yao isemayo mwanamke ni vazi la ndani.

Tunatengeneza wenyewe na kuuza bidhaa zetu kulingana na mahitaji ya mwanamke kuhusu urembo wa vazi la ndani ndio maana tumekuja na MSANII MAMA NAIRO ili kutambulisha bidhaa zetu kwa jamii .

Kwa upande wake wake MAMA NAIRO,ameshukuru kwa Ubalozi huo akidai kwamba huo ni ubalozi wa tatu kulamba  na kueleza kuwa CASSANDRA LINGERIE hawatajutia na maamuzi yao ya kumpatia ubalozi na amejipanga kufanya vurugu zote ili kuwabadilisha wanawake wavae vazi zuri la ndani na kuongeza mvuto kwenye mahusiano.

"Tangu nimeanza kufanya uchekesheji huu ni ubalozi wangu wa tatu ninayofuraha kuwaambia kuwa nitaitendea haki CASSANDRA LINGERIE mpaka mtajuta kunipa ubalozi nitahakikisha kila mwanamke, kila mama na kila msichana anavaa nguo nzuri na bora kutoka CASSANDRALINGERIE"

"Nawataka wanawake wote mniunge mkono ili kuongeza mvuto ndani ya nyumba" .





.......Ends...






Post a Comment

0 Comments