CRDB YAWAZAWADIA WATEJA, MAWAKALA KASKAZINI, PIKIPIKI, TV NA SIMU JANJA
...Washindi wajishindia Samsung, televisheni ya inchi 65, huku benki ikitaja zaidi ya mawakala 6,000
Na Joseph Ngilisho | ARUSHA
BENKI ya CRDB imeendelea kuimarisha uhusiano na wateja wake pamoja na kuwapa motisha mawakala wake, baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa robo ya kwanza ya kampeni ya Bonge la Wakala katika Kanda ya Kaskazini.Kwa upande wa mawakala, Albert Clement Peter wa Tawi la Tanga, Rose Mosha wa Usa River na Douglas Kimario wa Tengeru kila mmoja alijishindia pikipiki mpya, kutokana na kufanya vizuri katika kampeni hiyo.
Sadat alisema kampeni ya Bonge la Wakala inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kibenki kupitia mawakala, huku ikiendelea kuwapa wateja na mawakala motisha ya kuongeza matumizi ya huduma hizo.
Aliwahimiza wateja kutumia mtandao wa zaidi ya mawakala 6,000 wa CRDB waliopo katika Kanda ya Kaskazini, akieleza kuwa huduma hizo zinawawezesha kupata huduma za kifedha kwa urahisi, haraka na karibu na maeneo yao bila kulazimika kufika mara kwa mara kwenye matawi ya benki.
Aidha, aliwataka mawakala kuendelea kuboresha huduma, kuongeza ufanisi na kuimarisha mahusiano na wateja ili kuongeza idadi ya miamala na nafasi za kunufaika na zawadi zinazotolewa kupitia kampeni hiyo.
Alisema bado kuna fursa kwa wateja na mawakala wengine kushiriki na kujishindia zawadi mbalimbali, ikiwemo zawadi kubwa ya Sh milioni 10.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wateja, mawakala, mameneja wa mikoa ya Arusha pamoja na watumishi wa CRDB kutoka Ofisi ya Kanda ya Kaskazini
Ends
















Post a Comment