Breaking🔥

ADO AMTAKA NCHIMBI ,AMPIGA SIKU SABA KATAMBI KUELEZA ALIPO VINGINEVYO KUIBURUZA MAHAKAMANI SERIKALI

ADO SHAIBU AMPIGA SIKU SABA KATAMBI KUHUSU NCHIMBI

Na Joseph Ngilisho | Kahama

MBUNGE wa Jimbo la Tunduru Kaskazini na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi, kutoa taarifa ya wazi kuhusu mahali alipo aliyekuwa Makamu wa Rais na kiongozi wa zamani wa CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi, akimpa muda wa wiki moja kufanya hivyo.

Ado alitoa kauli hiyo Septemba 12, 2026, wakati akihitimisha ziara yake katika Mkoa wa Kahama, ambako alikutana na wenyeviti na makatibu wa chama ngazi ya mikoa, kabla ya kuzungumza na wananchi wa Kata ya Kagongwa.

Katika mkutano huo, Ado alieleza wasiwasi wa chama chake kuhusu kutokuwepo kwa taarifa za wazi kuhusu hali na mahali alipo Dk. Nchimbi, ambaye awali alijiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais na baadaye kufukuzwa uanachama wa CCM.

Alisema Serikali, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, ina wajibu wa kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu suala hilo, akimtaka Waziri Katambi kuhakikisha taarifa hiyo inatolewa ndani ya siku saba.

“Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, ndani ya wiki moja, atuambie Dk. Nchimbi yuko wapi na hali yake ikoje,” alisema Ado.

Alisema endapo Serikali itashindwa kutoa taarifa hiyo ndani ya muda alioutoa, ACT-Wazalendo iko tayari kuchukua hatua za kisheria kwa kufikisha suala hilo mahakamani ili kulazimisha Serikali kutoa maelezo kuhusu mahali alipo na hali ya kiongozi huyo.

Ado alisema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu jambo hilo na kuondoa sintofahamu inayoweza kujitokeza kutokana na kukosekana kwa taarifa rasmi.

Ziara ya Ado katika Mkoa wa Kahama ilihusisha mikutano na viongozi wa chama pamoja na wananchi, ikiwa ni sehemu ya shughuli za ACT-Wazalendo za kuimarisha chama na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi.

Ends...

Post a Comment

أحدث أقدم