LUKUMAY APEWA HADHI YA KIONGOZI MKUU KONGAMANO LA UMOJA WA MATAIFA,GENEVA

LUKUMAY ANG'ARA KONGAMANO LA UMOJA WA MATAIFA NCHINI GENEVA

Na Joseph Ngilisho-Arushadigital 

GENEVA, USWISI: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Dkt. Johannes Lembulung Lukumay (Mb), ameendelea kuiwakilisha Tanzania kimataifa baada ya kushiriki kama mmoja wa viongozi wakuu wa jopo la kimataifa (International Panellist) katika Kongamano la Umoja wa Mataifa linalojadili udhibiti wa madhara yatokanayo na majeraha ya ubongo na mfumo wa mishipa ya fahamu (Traumatic Brain Injury and Nervous System Injuries).

Ushiriki wa Dkt. Lukumay katika kongamano hilo linalofanyika jijini Geneva, Uswisi, unalenga kuchangia uzoefu wa Tanzania katika kuimarisha sera, kinga na huduma za afya zinazohusu majeraha ya ubongo na mfumo wa fahamu, sambamba na kujifunza mbinu bora zinazotumiwa na mataifa mbalimbali duniani.

Ends

Post a Comment

Previous Post Next Post