BAKWATA YAMTIMUA SHEIKH WA MKOA WA DAR NI YULE ALIYELALAMIKIWA NA MDADA KUMPA UJAUZITO NA KUMTELEKEZA, SHEIKH ABBAS ACHUKUA MIKOBA KWA MUDA

 BAKWATA YAMSIMAMISHA SHEIKH WA DAR ES SALAAM, KAWAMBWA ATENGULIWA

By Arushadigital-Dar Es Salaam

Baraza la Ulamaa la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limefanya kikao cha dharura leo Julai 14, 2026 chini ya uenyekiti wa Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Ali Khamis Ngeruko, na kuazimia kumsimamisha kazi Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni mienendo inayokiuka misingi na maadili ya uongozi wa taasisi hiyo.

Katika maamuzi yaliyofikiwa na kikao hicho, Sheikh Walid Alhad Omar Kawambwa ametenguliwa rasmi nafasi yake ya Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, hatua inayokuja baada ya Baraza kubaini uwepo wa ukiukwaji wa misingi ya uongozi inayosimamiwa na BAKWATA.

Sheikh Ngeruko, ambaye pia ni Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania, aliongoza kikao hicho cha dharura kilicholenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji na nidhamu ya viongozi wa taasisi hiyo.

Kufuatia uamuzi huo, Baraza limemteua kwa muda Sheikh Abbas Ramadhani kukaimu nafasi ya Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam. Sheikh Abbas ni mjumbe wa Baraza la Masheikh Mkoa wa Dar es Salaam na pia ni Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mtoro.

BAKWATA imeeleza kuwa hatua hiyo inalenga kulinda heshima, uwajibikaji na misingi ya uongozi bora ndani ya taasisi hiyo, huku ikiendelea kusimamia maadili na taratibu zake za kiutendaji.

Post a Comment

Previous Post Next Post