MAREKANI YAMPIGA STOP MAFWELE KUINGIA NCHINI MWAKE,YAMHUAISHA NA MAKOSA YA UKIUKWAJI WA HAKI ZA KINADAMU

 MAREKANI YAMPIGA MARUFUKU KAMISHNA WA POLISI TANZANIA

By Arushadigital

Idara ya Serikali ya Marekani imemtaja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania (TPF), Faustine Jackson Mafwele, chini ya Kifungu cha 7031(c) kwa madai ya kuhusika katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Hatua hiyo inamzuia Mafwele kuingia nchini Marekani, huku serikali ya Marekani ikieleza kuwa imefikia uamuzi huo kutokana na taarifa za kuaminika kuhusu matukio ya unyanyasaji yaliyodaiwa kufanywa dhidi ya raia wa kigeni waliokuwa nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwaka mmoja uliopita baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania walidaiwa kuwakamata, kuwatesa na kuwafanyia unyanyasaji wa kingono raia wa Uganda Agather Atuhaire pamoja na raia wa Kenya Boniface Mwangi waliokuwa jijini Dar es Salaam kufuatilia kesi ya mahakamani ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu.

Marekani imeeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya msimamo wake wa kuwawajibisha watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ukiukwaji wa haki za binadamu duniani.

Ends

Post a Comment

0 Comments