CCM YAPUUZA MAAGIZO YA MSAJILI KUJIELEZA KUHUSU KAULI YA CHATANDA?
Na Joseph Ngilisho|Arushadigital
CCM ililimwa barua yenye maelekezo kuwa hadi Mei 29, 2026 iwe imewasilisha ufafanuzi rasmi kufuatia kauli ya Chatanda aliyesema kuwa angepewa hata dakika moja ya kuongoza nchi, angeimaliza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kauli iliyozua mjadala mkubwa ndani na nje ya uwanja wa siasa.
Kupita kwa tarehe hiyo ya mwisho kumeifanya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa kitovu cha tahadhari ya wadau wa siasa, huku wananchi na wachambuzi wakisubiri kujua iwapo CCM imewasilisha majibu yake au kama hatua nyingine za kisheria na kiutawala zitachukuliwa.
Katika siku za hivi karibuni, suala hilo limeendelea kujadiliwa kwa mapana kwenye mitandao ya kijamii, ambapo wengi wanahoji ukimya uliopo kutoka kwa chama hicho pamoja na mamlaka husika baada ya muda wa utekelezaji wa agizo kumalizika.
Hadi sasa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haijatoa taarifa rasmi kwa umma kuhusu hatua zilizofikiwa, hali inayoongeza hamu ya kujua hatima ya suala hilo ambalo limevuta hisia za wadau wengi wa siasa nchini.
Ends...
