BASI LA KIDIA ONE LANASWA NA POLISI LIKIWA NA SHEHENA NZITO YA BANGI NAMANGA,WAWILI MBARONI POLISU YAMSAKA TAJIRI NA MWENYE MZIGO

POLISI NAMANGA WANASA SHEHENA YA BANGI KATIKA BASI LA ABIRIA, WAWILI WAKAMATWA

Arushadigital-NAMANGA

Maafisa wa Polisi mpakani mwa Kenya na Tanzania katika eneo la Namanga, Kaunti ya Kajiado, wamenasa shehena ya bangi iliyokuwa imefichwa ndani ya buti ya basi la abiria la kampuni ya Kidia One kutoka nchini Tanzania.

Taarifa zinaeleza kuwa bangi hiyo ilikuwa ikisafirishwa kwa kutumia basi hilo lililokuwa katika safari ya kawaida kutoka Dar es Salaam kuelekea jijini Nairobi, kabla ya kukamatwa katika kituo cha ukaguzi mpakani.

 

Katika operesheni hiyo, watu wawili waliokuwamo ndani ya basi hilo walikamatwa na wanashikiliwa na Polisi wa Kenya kwa mahojiano zaidi kuhusiana na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Hata hivyo, Polisi wamesema kuwa msako mkali unaendelea kumtafuta mhusika mkuu aliyekuwa akitarajiwa kupokea mzigo huo jijini Nairobi, huku wakibainisha kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini mtandao mzima uliokuwa nyuma ya tukio hilo.





Ends..

Post a Comment

0 Comments