SUALA LA POLEPOPE LAIBUA MAPYA ,AFISA WA POLISI ATAJWA MAHAKAMANI

 By Arushadigital 


Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imepanga Oktoba 16, 2025 kutoa uamuzi juu ya maombi ya Jamhuri wajibu maombi ya kutaka kuwahoji maswali ya dodoso Wakili Peter Kibatala na Godfrey Polepole,

Hatua hiyo inakuja baada ya Wakili wa wajibu, Faraji Nguka kuieleza mahakama mbele ya Jaji Salma Maghimbi ya kwamba wanaomba kumuhoji Kibatala na Godfrey kutokana na mkanganyiko kwenye kiapo kinzani.

Hata hivyo, maombi hayo yamepigwa na Wakili Kibatala akisema kuwa endapo kama mahakama itaruhusu kufanya hivyo basi italazimika kutoa nafasi kwa pande zote mbili kwa kuwa wote wana haki ya kufanya hivyo

Pia mawakili watashindwa kuwawakilisha vvema wateja wac kwa sababu watakuwa na kofia mbili na pia haoni jia nzuri ya upande wa Jamhuri zaidi ya kutaka kuchelewesha kesi hiyo liyofunguliwa chini ya hati ya dharura

Kutokana na mvutano huo, Jaji Salma Maghimbi ameahirisha <esi hiyo hadi Oktoba 16, 2025 kwa ajili ya kutoa uamuzi kisha kuendelea na maombi ya msingi

Maombi ya msingi katika kesi hiyo yamefunguliwa na Polepole <upitia Wakili Kibatala aliyeiomba mahakama itoe amri ya kwamba Polepole afikishwe mahakamani ama mamlaka ziseme ni wapi alipo



Post a Comment

0 Comments