DEREVA BODABODA ADAIWA KUMUUA MKE WAKE ARUSHA
Dereva bodaboda anayefahamika kwa jina la Taramael Emanuel (29), mkazi wa Kitongoji cha Mringa, Kata ya Olorien, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe, Marthe Pius.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kutekeleza tukio hilo la kikatili, Taramael alikimbilia Kituo cha Polisi cha Ngaramtoni na kujisalimisha mwenyewe.Kwa sasa anahojiwa ili kubaini mazingira na chanzo cha mauaji hayo.
Kwa mujibu wa rafiki wa marehemu, matatizo katika ndoa hiyo yalianza siku za karibuni na yaliongezeka Jumapili iliyopita walipokuwa wakielekea kanisani.
Tukio hili limeacha simanzi kubwa miongoni mwa wakazi wa Mringa, ambao wamesema hawakutarajia mzozo wa kifamilia kufikia hatua ya mauaji.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa uchunguzi wa awali unaendelea, huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
0 Comments