RAIA APIGWA RISASI MCHANA KWEUPE AKIINGIA OFISINI NA KUFA ,WAUAJI WATOWEKA NA PIKIPIKI

By arushadigtal -Dar Es Salaam 

Siku ya Leo tarehe 18 Julai, majira ya saa tano na nusu asubuhi eneo la Kinondoni Makaburini, Dar es Salaam, Alptekin Zeynelabidin Aksoy (52) Raia wa Tanzania mwenye asili ya Uturuki ameuawa baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu ambao walikuwa wakitumia usafiri wa pikipiki. 


Wahalifu hao inadaiwa hawakuchukua kitu chochote baada ya tukio hilo.


Taarifa inasema Alptekin Zeynelabin alishuka kwenye gari lake na kabla ya kuingia ofisini kwake alishambuliwa kwa risasi na kupoteza maisha. Uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo umeanza na Jeshi limetoa onyo kali kwa wote waliohusika kwa sababu zozote zile watakamatwa na kuingizwa kwenye mkondo wa sheria kwa hatua zaidi. #EastAfricaTV

Post a Comment

0 Comments