INASIKITISHA! WIVU WA MAPENZI WAMTOA ROHO MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AJINYONGA KWA SHUKA NI BAADA YA KUKUTA MESEJI YA MAPENZI KWENYE SIMU YA MPENZI WAKE!!

 MWALIMU ADAIWA KUJINYONGA TANGA KISA WIVU WA KIMAPENZI.


By arushadigtal -TANGA

Mwalimu Enock Johnson Peter (32) wa Shule ya Msingi Potwe wilaya ya Muheza mkoani Tanga amefariki dunia nyumbani kwake ikielezwa amekutwa amejinyonga na shuka, huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.


Akizungumzia tukio hilo, Mratibu Elimu Kata ya Pongwe Rajabu Msuya leo Jumatano Julai 16, 2025 alifika shuleni hapo kwa ajili ya kikao na walimu wa shule hiyo ya Potwe ambapo walimu wote walikuja kwenye kikao ispokuwa Enock hakuwepo.


Amesema baadaye alipotumwa mwanafunzi kwenda kumuita, aligonga mlango bila kuitikiwa na alirudisha majibu kuwa hakuna mtu. Hivyo ilimlazimu kumwagiza mwalimu mwingine kwenda kumwangalia mwenzao, ambapo na yeye alikosa majibu, lakini aliamua kuchungulia dirishani na kubaini alikuwa amejinyonga.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema tukio hilo lilitokea Jumanne ya Julai 15, 2025 katika Kata ya Potwe na uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo ni wivu wa kimapenzi.


Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo Abdulrazaq Kikungo amesema siku mbili kabla ya mwalimu huyo kujinyonga aligombana na mwenzi wake na kutishia kumuua kwa kumchoma kisu baada ya kukuta meseji za kimapenzi kwenye simu ya yake.


Mwili wa mwalimu utaagwa leo Jumatano shuleni hapo na kusafirishwa kupelekwa nyumbani kwao Ngara Kagera kwa ajili ya shughuli za mazishi.

Post a Comment

0 Comments