WIKI YA AZAKI YAZINDULIWA ARUSHA,ASASI ZAISHUKURU SERIKALI KUZISHIRIKISHA MPANGO WA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050

Na Joseph Ngilisho ARUSHA


 ASASI za kiraia (AZAKI)  zimeishukuru serikali kwa kuwashirikisha katika utoaji wa mawazo katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na kuhakikisha sekta ya elimu nchini inakuwa ni moja ya sekta za kimapinduzi, ili kusaidia  utekelezaji wa dira uendane na wakati ikiwemo matumizi ya Tehama. 



Hayo yalisemwa leo June 1,2025 Jijini Arusha na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Justice Rutenge wakati akizungumza na wanahabari kuhusu wiki ya Azaki inayoanza Juni 2 hadi June 6,2025 ambapo Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji ,Profeaa Kitila Mkumbo atahudhuria mkutano huo unaoshirikisha washiriki 800 hadi 900.


Rutenge alisema ushirishwaji wa azaki katika utoaji mchango wa Dira ya Taifa 2050 ni mkubwa na wametoa mapendekezo yao zaidi katika suala zima la elimu hususan katika matumizi ya teknolojia ya Tehama ili kuwezesha wanafunzi kuhakikisha wanapambana na kasi ya teknolojia inayokua kwa kasi Duniani. 


"Tunashukuru serikali kwa kushirikiana nasi haswa katika uundwaji wa dira na kukuza uchumi endelevu na sisi tumesema sekta ya elimu ni muhimu katika kuhakikisha inakua ikiwemo kwenda na kasi ya Tehama inayokuwa ziadi Duniani,"alisema


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Azaki, CPA Mercy Silla  alisema mashirika hayo yanajivunia miaka saba tangu yalipoanzishwa lengo kubwa ni  kuwaleta pamoja wadau wa sekta ya Azaki kufanya mijadala mbalimbali ya maendeleo kwa mustakabali wa nchi yetu Tanzania. 


"Kila mwaka tuna utaratibu wa kuangazia mambo mbalimbali na kuweka sawa Maudhui ya wiki ya Azaki na mwaka huu tutaangazia mchakato mzima wa dira ya Taifa na tunajivunia maendeleo kwani ni wakati sasa wakuangalia jinsi ya kujiendesha mashirika haya wenyewe pasipo kutegemea wahisani lazima tuweke mbinu za kujikwamua wenyewe,"alisema


Mkurugenzi mkazi, CBM International ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati za Asasi za Kiraia, Nesia Mahenge alisema wiki hiyo inalenga kutatua changamoto ambazo zipo katika azaki za kiraia na kuona ni namna gani zinatatuliwa.

Post a Comment

0 Comments