LATRA YAONYA WAMILIKI WA MABASI WANAOAJIRI WAHUDUMU WA MABASI WASIOPITIA VYUO VYA UDEREVA ,YAPONGEZA WAHITIMU 74 WA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

Na Joseph Ngilisho- ARUSHA 


MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri, Ardhini (LATRA),imewata wamiliki wa mabasi Mkoani Arusha,kuhakikisha wanaajiri madereva na makondakta waliopitia mafunzo kutoka kwenye vyuo udereva vinavyotambuliwa na serikali .


Akiongea  wakati wa kuhitimisha mafunzo ya wiki moja ya wahudumu wa mabasi Makondakta na madareva kutoka makampuni mbalimbali ya usafirishaji na wasio na makampuni wapatao 74 katika chuo cha ufundi Arusha.

Afisa wa LATRA Mkoa wa Arusha, Omari Ayubu  alisema sheria ya usafirishaji inasema mwajiri ama mmiliki wa chombo cha usafiri haruhusiwi kuajiri dereva ama kondakta ambaye hajapitia mafunzo katika sekta ya usafirishaji,hivyo alionya wamiliki watakaokwenda kinyume nansheria hiyo.


Ayubu alikipongeza chuo cha ufundi Arusha kwa kutekeleza takwa la sheria ya usafirishaji kwa kutoa mafunzo katika fani ya usafirishaji kwa Madereva na Makondakta wa mabasi ya umma.


"Sheria inaelekeza kwamba,msafirishaji haruhusiwi kumwajiri kondakta au dereva ambaye hajapata mafunzo ama hajasajiliwa kutoka mamlaka ya  LATRA na kwamba mwajiri atakaye kwenda kinyume na sheria hiyo atachukuliwa hatua"


Alisema ,hatua hiyo inalenga kuboresha sekta  ya usafirishaji kwa kuongeza ukaribu kwa abiria ili  mabasi hayo yaweze kuwa na kivutio cha wageni mbalimbali wanaoingia nchini wakiwemo watalii.


Aliwataka wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri kwa kuyatumia mafunzo hayo kwenda kuboresha sekta ya usafirishaji hapa nchini na alitoa wito kwa wahudumu wengine ambao wanafanya kazi kinyume cha sheria , kuhakikisha wanajiunga na shule za udereva ili kupata mafunzo stahiki.







Awali mkuu wa chuo cha Ufundi  Arusha ATC ,Mussa Chacha,alisema tangu wameanza kutoa mafunzo hayo ya wahudumu wa mabasi kumekuwa na mwitikio mkubwa na yanasaidia kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.


Chacha aliishukuru Latra kwa kukiamini chuo hicho na kukipa jukumu kubwa  kuwa miongoni mwa vyuo vinavyotoa mafunzo bora katika sekta ya usafirishaji nchini.


"Chuo chetu kinatarajia matokeo chanya kwa wahitimu wa mafunzo haya ambao ni wahudumu wa mabasi ,tutaendelea kuwajengea uwezo wahudumu wengine watakaokuja kujifunza ili kutimiza azma ya serikali ya kuboresha sekta ya usafirishaji kwa kuwa na wahudumu wenye Lugha nzuri kwa wateja wao"


Naye mkufunzi wa udereva cha chuo hicho cha Ufundi Arusha na mkuu wa idara ya uhandisi wa Magari ,mhandisi David Mtunguja alisema kuwa wahitimu 74 wamepata mafunzo ya wiki moja na kutunukiwa cheti kitakachowatambulisha mafunzo hayo.


Katika risala ya wahitimu hao iliyosomwa na mhitimu Katrona Marandu walisema wamejifunza mada mbalimbali  takribani tano ambazo ziwewawezesha kuelewa utoaji wa  huduma kwa wateja,maadili kwa wahudumu,Huduma ya kwanza ,Masomo ya kuzima moto na. Utunzaji Data.


Walisema mafunzo hayo yamewaongezea ari ya kufanya kazi kwa ufanisi na  kuipenda dzi yao na wanaenda kuleta mapinduzi kwa kuiboresha sekta ya usafirishaji na kuipatia heshima kwa manufaa ya taifa la Tanzania.


Ends 



Post a Comment

0 Comments