SIASA ZA TAWALA MKUTANO WA MADAKTARI ARUSHA,RC MAKONDA RASMI KUNYAKUA JIMBO LA ARUSHA MJINI ,AMTAKIA HERI MAJALIWA RUANGWA ,MOLLEL ATAMBA SIHA AMEMALIZA KAZI

Na Joseph Ngilisho-ARUSHA


SIASA za kutakiana Heri kwenye majimbo zimetawala katika mkutano wa chama cha madaktari Arusha(M.A.T),ambapo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemwomba waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kumtakia kila la heri katika uchaguzi ujao.


Kauli hiyo ambayo ameitoa leo juni 18,2025 katika mkutano huo unaofanyika aicc Arusha,ni wazi kwamba Makonda ameingiza miguu yote kulinyakua jimbo hilo kutoka kwa mbunge wa Sasa Mrisho Gambo ambaye umaarufu wake umeendelea kuporomoka kutokana na mnyukano wa wawili hao unaoendelea.


Kadhalika Makonda amemtakia kila la heri  waziri Mkuu Kasimu Majaliwa katika jimbo lake la Ruangwa huku akisisitiza kuwa isingekuwa uchaguzi alikuwa amepania jiji la Arusha kuwa kama dubai kutokana na mipango aliyokuwa nayo.


"Mhe. Waziri Mkuu katika mipango bora iliyopo ya kulifanya jiji la Arusha kuwa kitovu cha utalii na sasa katika usafiri wa anga kwa kipindi cha miaka mitano Arusha ingekuwa ni kitu kingine ni vile tu kuna uchaguzi na tumebakiza siku chache". Amesema Makonda.


"Nasema hivi ni uchaguzi tu naimani waziri Mkuu amenielewa na mimi nikutakie kila lenye kheri Ruangwa na mimi usiache kunitakia kheri ili baada ya uchaguzi utakapo malizika na tutakapo kutana tufurahie kwa pamoja kuwa tulitakiana kheri". Amesisitiza Makonda.


Naye naibu waziri wa Afya Dr Godwin Mollel  alisema kuwa katika jimbo lake la SIHA amemaliza uchaguzi na kumtakia heri waziri Mkuu Majaliwa na kumuomba asiache kufika jimbo la Siha ili kuhakikisha kura zake zinaendelea kujaa.


"Mhe. Waziri Mkuu mimi ni kama M'bunge wa pili Ruangwa maana nimefika mara nyingi katika kuteleza majukumu katika sekta ya Afya nimejione kwamba umesha maliza na unasubilia kuongoza tena kwa miaka mitano na mimi pale Siha nimeshamaliza nasubilia kusheherekea na kuendelea kuchapa kazi". Amesema Mollel.


"Na kwa vile tunahitaji viongozi wanaochapa kazi na sio maneno nikutakie Mhe. Makonda kila la kheri pale ulipo panga kulitumikia taifa letu umefanya mengi katika uongozi wako kama Mkuu wa Mkoa na matunda yanaonekana". Ameongeza Mollel.

Kwa upande wake waziri Mkuu amewahamasisha wananchi kujitokeza kugombea nafasi yoyote ya uongozi kama haki yao ya msingi ya kila mwananchi. 


Aliwataka wananchi kutafakari lugha za wagombea iwapo kama zinafaa kwa ushawishi .


Ends..



Post a Comment

0 Comments