Na Joseph Ngilisho-ARUSHA
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametangaza fursa ya uwekezaji wa bandari kavu katika Jiji la Arusha kwa ajili ya kushughulikia makontena ya mizigo kutoka nje ya nchi yanayopitia bandari ya Tanga Fursa hiyo inalenga kupokea na kusafirisha mizigo kwa ufanisi zaidi kupitia njia ya reli.
Makonda ameyasema hayo leo Jumanne, Juni 17, 2025, katika hafla ya utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa uwanja wa michezo wa Jiji la Arusha na soko la machinga Amesema uhitaji wa bandari hiyo kavu umekuja baada ya hatua ya Serikali kuridhia maboresho ya reli ya Tanga- Arusha na kuongeza uwezo wake wa kusafirisha mizigo,.
Kwa mujibu wa Makonda, baada ya maboresho ya bandari ya Tanga, ambayo awali ilikuwa inahudumia meli ndogo pekee, sasa ina uwezo wa kuhudumia meli kubwa, jambo lililosaidia kuwapo kwa ongezeko la idadi ya malori yanayobeba mizigo kutoka bandari hiyo kuelekea Arusha kutoka 60 na kufikia zaidi ya 600 kwa siku. Hali hiyo imeongeza mzigo mkubwa kwa barabara za mkoa huo.
"Nilizungumza na Rais wetu kuhusu haja ya kuboresha reli yetu ya Tanga- Arusha, kuongeza uwezo wake na alipokea maoni hayo kwa mikono miwili. Tayari viongozi wa reli wameshafika na kazi imeanza," amesema Makonda.
Kitaifa Amesema reli hiyo ambayo awali ilikuwa na mwendo wa kilomita 30 kwa saa, baada ya maboresho itakuwa na uwezo wa kusafirisha kwa kasi ya hadi kilomita 70 kwa saa,
Lengo kuu ni kuharakisha usafirishaji wa mizigo kutoka Tanga hadi Arusha, yakiwamo makontena yanayoelekea nchi jirani za Afrika Mashariki.
"Sasa kazi hiyo ikiendelea, tunahitaji bandari kavu hapa Arusha kwa ajili ya kuhifadhi na kuchakata mizigo hiyo kabla ya kupelekwa maeneo mengine Hii ni fursa muhimu kwa wafanyabiashara na wawekezaji Njooni tujadiliane utaratibu na Ä·azi ianze," amesisitiza mkuu huyo wa mkoa.
Kitaifa uwanja wa michezo wa Arusha Jiji wenye thamani ya Sh 9.6 bilioni.
Alisema ujenzi huo unatekelezwa na Kampuni ya STC Construction Co. Ltd, na utakuwa na uwezo wa kuingiza zaidi ya watu 8,000 na kuendana na matarajio ya kuwa sehemu ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027.
"Uwanja huo wa kisasa utatumika mchana na usiku, utakuwa na viwanja vidogo vitatu vya michezo mingine kama wa pete na kikapu, vyumba vya kubadilishia nguo, vyoo zaidi ya 50 na maegesho ya magari zaidi ya 150. Pia utakuwa na mageti 12 kwa ajili ya kuingia na kutoka," amesema Dk Maduhu.
Akizungumzia ujenzi wa soko la machinga, amesema litajengwa eneo la Mrombo na kutekelezwa na Kampuni ya Suma JKT Construction
Kwa upande wake, Meneja wa Suma JKT Kanda ya Kaskazini Magharibi, Luteni Kanali Daudi Zengo amesema watahakikisha kazi ya ujenzi inakamilika ndani ya mwaka mmoja waliopangiwa, kuanzia sasa hadi Juni mwakani.
"Tunashukuru Serikali kwa kutupatia kazi hii. Kuanzia kesho tunaanza rasmi ujenzi, tumejipanga kuhakikisha tunakamilisha kwa viwango vinavyotakiwa,' amesema Zengo Katika hafla hiyo, watendaji wa kata zote 25 za Jiji la Arusha walikabidhiwa pikipiki 23 na bajaji mbili zenye thamani ya Sh106 milioni ili kuwasaidia katika utendaji wa kazi za kila siku.
Ends..
0 Comments