NAMELOCK ATIKISA ARUSHA AMSHUKURU RAIS SAMIA,APOKEWA KWA KISHINDO WAZEE WA KIMILA YA KIMASAIL WAMPA BARAKA NZITO TAZAMA, PICHA!

Na Joseph Ngilisho- ARUSHA 


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Namelock  Sokoine, amemshukuru mwenyekiti wa ccm Taifa  rais  Samia Suluhu Hasani kwa kumteua kushika wadhifa huo na kuwaomba wananchi kumuunga mkono katika kushiriki uchaguzi mkuu ujao.


Akipokewa kwa hamasa,nderemo, vifijo  na umati wa Wananchi jana alipowasili jijini Arusha na baadaye wilayani Monduli alipozaliwa, Namelock alisema nafasi aliyopewa na rais Samia ameheshimisha Mkoa wa Arusha.


Namelock alionekana mwenye furaha kubwa baada ya kushuhudia mapokezi makubwa kutoka kwa Wananchi wa Arusha,akapata wasaa wa kupanda jukwaani na kuhutubia  wakazi wa Wilaya Monduli na Viunga vyake ndani ya jiji la Arusha .


"Namshukuru kwa dhati ya moyo wangu Mwenyekiti wangu wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa heshima kubwa aliyoitoa kwa Mkoa wa Arusha kupitia nafasi ya Uongozi niliyonayo kwa sasa,


Kwa niaba ya wana-Arusha na Monduli kwa ujumla, naahidi kuitunza na kuilinda heshima hii kwa moyo wangu wote,na ninawaomba tuendelee kumuombea na kumuunga mkono Rais wetu kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo anayoyafanya ndani ya nchi yetu,” alisema Ndugu Namelock  kwa msisitizo.


Aidha,  Namelock aliwahimiza wananchi kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao kwa kusema: “Oktoba kazi ni moja tu, tusimame na Mama Samia, tumuunge mkono kwa vitendo ili kuendeleza maendeleo yanayoonekana kote nchini,na kwamba ahadi ya watu wa Monduli ni ile ile 2025 kura zote kwa Mhe.Rais Dkt Samia na Mgombea Mwenza Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi.


 Namelock pia alimaliza kwa kuweka msisitizo kuwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia umeendelea kuleta matumaini, mshikamano na dira ya maendeleo kwa Watanzania wote, hivyo kuna kila sababu ya kuendeleza mshikamano  ndani ya chama na kwa Taifa.













Ends..

Post a Comment

0 Comments