MWANDISHI AZINDUA CHOMBO CHA HABARI KWA KISHINDO,ACHANGIWA MAMILIONI PAPO HAPO,SERIKALI YAMWAGIA SIFA,YATOA NENO KWA JAMII YA WAFUGAJI!

Na Joseph Ngilisho-MONDULI

JAMII ya wafugaji waishio pembezoni , wameaswa kutumia vyombo vya habari kupaza sauti ili kufikisha kilio chao kwa serikali na kusaidia kutatuliwa changamoto ya migogoro ya Ardhi,mipaka na malisho.

Kauli hiyo imetolewa leo June 14,2025  na kaimu Mkurugenzi wa habari Maelezo, Rodney Thadeus wakati alipomwakilisha   naibu waziri wa utamaduni na Michezo,Hamis Mwinjuma katika hafla ya uzinduzi wa chombo cha Habari cha Oldonyo Media kinachomilikiwa na mwandishi wa habari, Juliana Laizer kutoka jamii ya wafugaji.

 

Hafla hiyo ilifanyika katika kata ya Lepurko ,Nanja wilayani Monduli Mkoa wa Arusha na kuhudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo wa jamii hiyo ambapo pamoja na mambo mengine ilifanikisha changizo la zaidi ya sh,milioni 20 kwa ajili ya kuunga mkono huduma  ikiwemo unhnuzi wa vifaa vya uendeshaji huku kamati ya maandalizi ikichanga zaidi ya sh,milioni 10.

Thadei ambaye alichangia kiasi cha sh,500,000 akimpongeza Mwandishi huyo wa habari kwa kuanzisha chombo cha habari cha mtandaoni akidai kitaongeza chachu na wigo wa upatikanaji wa habari kwa  wananchi  jamii hiyo kujieleza ,kuhamasika na kuelimika .


Aidha aliwataka viongozi,taasisi na mashirika ya umma, kutoficha habari bali wawape ushirikiano  wanahabari  ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kuwahabarisha wananchi ili wajue kinachoendelea ndani ya serikali yao katika kuwaletea maendeleo.


Kadhalika alionya vyombo vya habari visitumike kupotosha jamii, bali vitoe habari za uhakika kwa kusimamia misingi ,weledi wa uandishi wa habari  unaozingatia maadili na kuepuka kujiingiza kwenye mitego ya migogoro na chuki , hatua itakayoepusha kuleta taharuki hasa kipindi hiki ambacho taifa linaingia kwenye uchaguzi.


"Nimpongeze dada yetu Juliana kwa kuzindua chombo cha habari cha Oldonyo Media ni hatua nzuri, nitumie fursa hii kuwaomba waandishi wa habari kuhakikisha wanasimamia misingi na maadili ya uandishi wa habari ili kuakikisha tunachokiandika kinakuwa na maslahi mapana kwa jamii na kwataifa kwa ujumla "Alisema Thadei.


Awali Mkurugenzi wa Oldonyo Media,Juliana Laizer alisema kwa muda mrefu amekuwa na ndoto ya kuanzisha chombo cha Habari kutokana na uhitaji wa jamii ya kifugaji kupata chombo cha kusemea changamoto zao.


Alisema awali alikuwa akiibua na kuandika habari za wafugaji kupitia vyombo vingine vya habari ila hakupata upeo mkubwa wa kuzitangaza ndipo alipopata wazo la kuazisha chombo chake kwa lengo la kuwa na wigo mpana zaidi wa kuhabarisha jamii.


"Nimeamua kuanzisha chombo cha Habari nikitumia jina la kimasai la Oldonyo ikiwa na maana ya Mlima,nimeanzisha chombo hicho kwa lengo la kuibua na kuandika habari za jamii ya wafugaji waliopo pembezoni wasiofikiwa kirahisi "


Alisema awali alifanikiwa kuibua migogoro ya ardhi,mipaka na malisho ambayo ilipata kutatuliwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kata ya Sepeko na Engaruka .


Alisema pamoja na mambo mengine chombo hicho cha habari atakitumia kuhamasisha jamii hiyo ya kifugaji kupeleka watoto wao shule,kupinga ukeketaji pamoja na kuielimisha jamii hiyo katika masuala mbalimbali ya kijamii .



Katika hafla hiyo ya uzinduli na harambee alikusudia kupata kiasi cha sh,milioni 50 lakini alifanikisha kupata michango mbalimbali iliyofikia kiasi cha zaidi sh,milioni 20 .


Katika hatua nyingine Laizer alishukuru kwa kupata uteuzi kutoka chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) kuwa afusa habari wa chama hicho,ikiwa ni jitihada zake za kuibua na kuandika habari za wafugaji zinazofanikisha kupunguza changamoto za wafugaji nchini.


Naye Diwani wa Kata ya Lepurko Yonas Laizer alisema jamii ya kifugaji imekuwa ikielimika kupitia vyombo vya habari hivyo kuanzishwa kwa chombo hicho kutachochea zaidi kwa jamii yao kusaidia kuwapa wigo mpana wa kupaza sauti na kupunguza changamoto za wafugaji.


"Ninacho wasihi jamii ya kifugaji kutumia vyombo vya habari kuelimika na kuboresha maisha yao na watumie vyombo vya habari kujinufaisha kwa kutangaza bidhaa zao za mifugo na pia kuhamasisha kuwapeleka watoto wao shule"









Ends.....









Post a Comment

0 Comments