HUYU HAPA MANUSURA PEKEE WA AJALI YA NDEGE INDIA ,WENZAKE 241WALIFARIKI DUNIA

Arushadigtal,AHMEDABAD, India 

Viswashkumar Ramesh, raia wa Uingereza mwenye asili ya India, ndiye abiria pekee aliyepona katika ajali ya ndege ya Air India iliyokuwa ikielekea London kutoka Ahmedabad. Akiwa kitandani katika Hospitali ya Civil jijini Ahmedabad, Ramesh ameeleza kwa uchungu jinsi alivyopitia sekunde za mauti kabla ya kujiokoa.

"Ndege haikupaa vizuri, ilikuwa kama inateleza hewani tu," alisema katika mahojiano na DD News, Ijumaa. "Sekunde chache tu kabla ya kugonga jengo na kulipuka, nilihisi tunaporomoka." Ramesh, aliyekuwa kwenye kiti cha 11A kando ya dirisha, alisema upande wake wa ndege ulipata uharibifu mkubwa, na aliona ufa kwenye sehemu ya fuselage karibu na kiti chake.

"Nilidhani nimekufa. Lakini nilipoona ufa huo, nilijifungua mkanda, nikatumia mguu wangu kusukuma nikapitia hapo na kujivuta nje," alieleza.

Ajali hiyo imezusha maswali kuhusu usalama wa ndege, huku baadhi ya wataalamu wakitaka hatua kali zichukuliwe. Wataalamu wanabishana kati ya umuhimu wa ukaguzi mkali wa ndege kabla ya kuruka na mafunzo ya kina kwa marubani na hatua za dharura kama njia bora ya kuzuia ajali kama hii.

#

Post a Comment

0 Comments