By arushadigtal-DODOMA —
Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, George Mcheche Masaju, kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.
Masaju anachukua nafasi ya Prof. Ibrahim Hamis Juma, ambaye amestaafu rasmi baada ya kulitumikia taifa katika nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka saba.
Prof. Juma aliteuliwa kuwa Jaji Mkuu Septemba 2017 na Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli, akichukua nafasi ya Jaji Mohamed Chande Othman. Alizaliwa Juni 15, 1958 mjini Musoma, mkoani Mara, na ana shahada kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), pamoja na masomo ya juu katika taasisi kadhaa za kimataifa zikiwemo SOAS – University of London, Chuo Kikuu cha Lund (Sweden), na Chuo Kikuu cha Ghent (Ubelgiji).
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, ikieleza kuwa hafla ya uapisho wa Jaji Mkuu mpya itafanyika Juni 15, 2025, kuanzia saa 4:00 asubuhi katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
0 Comments