Na Joseph Ngilisho ARUSHA
WANAHISA wa Benki ya CRDB wanatarajiwa kunufaika na gawio la Sh. 65 kwa kila hisa kwa mwaka 2025 baada ya benki hiyo kupata faida ya sh, bilioni 551 baada ya kodi kwa mwaka 2025 ukilinganisha na faida ya mwaka jana 2024 sh, bilioni 450.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha leo Mei,14,2025, kuelekea mkutano mkuu wa 30 wa benki ya CRDB wenye kauli mbinu 'miaka 30 ya ukuaji pamoja ' unaotarajiwa kufunguliwa na makamu wa rais dkt Philipo Mpango Mei 17,2025 katika kituo cha AICC jijini Arusha ukitanguliwa na semina maalum kwa wanahisa ambayo itafanyika Ijumaa Mei 16,2025.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB, Dk. Ally Laay, alisema kutokana na faida hiyo bodi ya wakurugenzi imependekeza gawio la sh,65 kwa kila hisa ,ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 30, ukilinganisha na gawio la mwaka jana 2024 la sh,50.
Alisema iwapo gawilo hilo litaidhinishwa na wanahisa ,benki hiyo itatoa gawio la jumla ya sh,bilioni 169.8 kwa wanahisa wote mwaka huu 2025 na hivyo kuvunja rekodi zilizopita.
"Kutokana na faida hiyo, Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa wa benki uliopangwa kufanyika Jumamosi meib17,2025 katika kituo cha Aicc jijini hapa, pamoja na mambo mengine, unatarajiwa kupitisha pendekeo hilo la ongezeko la gawio kwa hisa linalotokana na benki kuendelea kupata matokeo mazuri sokoni".
Alisema ajenda mbalimbali zitajadiliwa katika mkutano huo, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa wajumbe huru wa bodi, kuteua wakaguzi wa hesabu, kujadili na kupokea Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi, Taarifa ya Hesabu Zilizokaguliwa na gawio kwa mwaka 2025.
Dkt. Laay aliongeza kuwa, mkutano huo pia utafanyika kwa njia mseto ili kutoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki kwa njia ya kidigitali.
Alisema kupitia mtandaoni, wanahisa wataweza kujiunga kuanzia saa 2:00 asubuhi kupitia tovuti ya benki hiyo au mfumo wa benki hiyo waliopakua katika simu au kompyuta zao.
"Tumeweka mwongozo wa jinsi ya kushiriki mkutano mkuu kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yetu, mitandao yetu ya kijamii, pia maelekezo yametumwa kwa ujumbe mfupi kwa wanahisa," alisema Dkt. Laay .
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema thamani ya benki ya crdb imekuwa na kufikia sh,trilioni 17.6 hadi robo ya kwanza ya mwaka kutoka januari hadi machi 25,2025 na kuweza kupata faida ya sh,bilioni 173.
Akizungumzia mkakati wa kufungua matawi ya benki hiyo nje ya nchi, alisema kuwa benki hiyo imefanikiwa kuwa tawi katika nchi ya Burundi tawi linalofanya vizuri zaidi na kuwa benki kinara katika nchi hiyo.Pia alisema benki hiyo imefanikiwa kuingia nchi ya DR Kongo na Tayari imefungua matawi katika miji ya Kinsasa na Lubumbashi ambayo yanaendelea vizuri.
Alisema mpango mwingine ni kufungua tawi katika nchi ya Dubai na tayari wamepata kibali na mchakato wa kupata eneo la kufungua tawi la CRDB unaendelea,huku mpango mkubwa ni kufungua matawi katika nchi mbalimbali za Afrika unaendelea.
Katika hatua nyingine alisema thamani ya hisa ya benki hiyo imeongeza baada ya kuwepo kwa hamasa kubwa kwa ununuzi wa hisa kwa mtu mmoja mmoja hii ni kutokana na maboresho ya miundo mbinu,ubunifu mkubwa kuongezeka kwa mapato na kubana matumizi .
Aidha Nsekela alitumia fursa hiyo pia kuhamasisha wanahisa wa Benki ya CRDB kujitokeza kwa wingi kwa kuwa ushiriki wao utawezesha Bodi na Menejiment kupata maoni yao ya namna bora ya kuboresha huduma za kibenki.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Crdb Foundation bi Tulli Esther,alisema kuwa kabla ya mkutano mkuu benki hiyo itafanya matukio mbalimbali kwa jamii ikiwemo kukabidhi madarasa maalumu katika shule ya Uswaa iliyopo wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.
Pia alisema crdb itakabidhi madarasa kwa shule iliyopo wilayani Arumeru mkoa wa Arusha pamoja na kutoa semina kwa vijana na wanawake katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
Benki ya CRDB pia ilizindua Ripoti yake ya mwaka 2024 inayoonesha maendeleo makubwa ya kifedha,kiutendaji,na Kijamii yaliyopatikana katika kipindi hicho.
Ends .
0 Comments