RED GOLD YATAMBULISHA BIDHAA MPYA YA MWENDO KASI TAZAMA PICHA HAPA !

 Na Joseph Ngilisho-ARUSHA



KAMPUNI ya Kuzalisha Tomato Sauce  na bidhaa zingine ya Darsh Industries co LTD ya jijini Arusha,imetambulisha bidhaa mpya ya pilipili aina ya Mwendo kasi ambayo imeleta mapinduzi ya radha  nzuri kwenye chakula kiasi cha kupewa jina la msisimko wa mtaa.

Akitambulisha bidhaa hiyo ya Mwendo Kasi ,katika mkutano wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania NBAA na BOT unaofanyika Aicc jijini Arusha ,afisa mauzo wa kampuni hiyo,Dipak Makwana alisema kuwa bidhaa hiyo ni miongoni mwa bidhaa 50 zinazozalishwa na kampuni hiyo ikitumia nambo ya RED GOLD.



Dipak alijipambanua kuteka soko la bidhaa zake hapa nchini na nchi jirani ambapo pamoja na mambo mengine alisema bidhaa zake zimependwa zaidi na kutumiwa kwenye mighahawa ,mahoteli pamoja na majumbani.

"Tumekuja hapa Aicc katika mkutano wa NBAA na BOT kama wadhamini na tumepata fursa ya kutangaza bidhaa zetu pendwa ikiweno pilipili ya mwendo Kasi ,tunazalisha bidhaa zaidi ya 50 ikiwemo Peanut Butter,Tomato Paste Mixed Fruit jam ,Mango Pickle,Tea Masala ,Chili Ketchup nk na tutakuwepo hapa kwa siku tatu"Alisema Dipak.



ALIONGEZA Kuwa.." huduma za bidhaa zetu ambayo tunatoa hapa Tanzania hakuna kona ambayo hatujafika tupo wilaya zote na tunauza hadi nchi za jirani kwa sasa"

Alisema sifa moja wapo ya bidhaa zao ni kutumia malighafi za  hapa nchini ikiwemo Nyanya na karanga zinazolimwa na wakulima wa hapa nchini na kwamba bidhaa zao hazikai muda mrefu sokoni.

Dipak aliwaomba watanzania kupenda kununua bidhaa  zinazozalishwa na wazawa hapa nchini ili waweze kuwaunga mkono wakulima ambao wamekuwa wakipata shida ya masoko pindi wanapoivisha  mazao yao.

ends....




Post a Comment

0 Comments