Na Joseph Ngilisho ARUSHA
GAVANA wa Benki Kuu Tanzania BOT, Emmanuel Tutuba amewataka wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania(NBAA) kutumia utaalamu wao kuboresha sekta wanazozisimamia ili zilete matokeo chanya na kutoa mchango mkubwa zaidi katika ukuaji wa uchumi.
Tutuba ameyasema hayo leo Jumatano Mei 28,2025 jijini Arusha, wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka 2025 wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) na BOT na kusisitiza usimamizi jumuishi wa mifumo ya kifedha ili kufahamu mifumo ya Kidigitali inayoendelea duniani.
"Kundi hili la wahasibu na wakaguzi wa hesabu linayofursa ya kufahamu Changamoto zikizopo katika sekta hiyo na kuzitafutia majawabu ili kuboresha ukuaji wa uchumi wetu wa Tanzania"
Alisema malengo ya serikali ya Tanzania yameendelea kufanya vizuri katika nyanja tofauti za usimamizi wa kifedha na kupelekea ukuaji wa uchumi .
"Mwaka jana uchumi wa Tanzania umekuwa kwa asilimia 5.5,mfumo wa bei umeshuka kwa asilimia 3.1 kwa mfano mfumko wa kidumia mwaka jana mwaka jana ulikuwa ni asilima 4.7 lakini sisi tulikuwa na asilimia 3.1 maana yake tumefanya vizuri zaidi kwenye ukuaji wa uchumi "
Alitoa rai kwa washiriki wa Mkutano huo kuhakikisha wanaboresha shughuli zao za kufunga hesabu vizuri,ukaguzi mzuri wa hesabu kwenye taasisi wanazozisimamia ili kutoa mchango mzuri zaidi katika ukuaji wa uchumi.
Akizungumzia mkakati wa kitaifa wa usimamizi wa uchumi wa Kidigitali unatekelezwa kwa miaka 10 ambao umezinduliwa na serikali mwaka jana 2024 ,alisema huduma za kifedha zinatakiwa kutumia mifumo ya kidigtali kurahisisha namna ya kuwafikia watu wengi na kutoa fursa kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya vijana.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA,CPA Pius Maneno alisema mkutano huo unalenga kuangazia utawala bora katika dhana za Kidigitali na kuhusisha wataamu kutoka taasisi zaidi ya tano wakiwemo Benki kuu ya Tanzania BOT.
CPA Maneno alisema katika mkutano huo ni mara ya 25 wamekuwa waliofanya mkutano nankileta manufaa na mwaka huu watajadili mada 11 ikiwemo mada ya ulinzi wa fedha katika mitandao.
Alisema kuna utaratibu mpya ambao umeanzishwa utakaowataka wakaguzi kutayarisha hesabu ambazo zitakuwa zimehifadhiwa NBAA.
"Mwaka 2021 tulibadilisha sheria ya NBAA kutaka wakaguzi wakikagua hesabu zije NBAA, lakini tulikumbana na Changamoto ,utakuta mtu anatengeneza hesabu tatu za kukaguliwa ,hesabu moja anapeleka benki na hiyo itakuwa imenona, inaonesha faida kubwa ,taarifa ya pili inakuwa ya kupeleka TRA na hiyo inakuwa finyu haina kitu ili asilipe kodi na taarifa ya tatu inakuwa ya kupeleka nyumbani kwake ikiwa sawa"
Alisema kwa sasa NBAA imekuja na mfuko mpya wa kutoa namba maalumu (control number) baada ya kuridhika na hesabu zilizokaguliwa ,hii itasaidia kudhibiti vishoka waliokuwa wanaofanya udanganyifu na mpango huo utaanza kutumika kuanzia julai mwaka huu.
Ends....
0 Comments