RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI WA NCHI ZA SADC

 RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI WA NCHI ZA SADC.

By arushadigtal


Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe.Paul Christian Makonda, leo 30 Mei, 2025 amefungua mkutano wa 33 wa mwaka wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliohudhuriwa na Wakuu wa Majeshi wa Nchi wanachama.




Katika hotuba yake, Makonda amekaribisha Wakuu hao kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika Mkoa huo na Mikoa jirani kama vile Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Arusha National Park, mbuga ya wanyama Tarangire, Mlima Kilimanjaro pamoja na Mbuga ya wanyama Serengeti.


Mkutano huo unaoongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob Mkunda, ulianza 26 Mei, na unatarajiwa kuhitimishwa 31 Mei, 2025.



Post a Comment

0 Comments