MADEREVA NA MAKONDAKTA WATAKIWA KURUDI DARASANI ,CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAPONGEZWA KUPIKA MADEREVA BORA, CHATAKIWA KWENDANA NA TEKNOLOJIA YA KISASA

 

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamishna msaidizi Mwandamizi wa polisi, William Mkonda ,amewataka madereva wa Magari  pamoja na makondakta kuhakikisha wanapitia Mafunzo katika chuo cha Ufundi Arusha ATC, pamoja na vyuo vingine vyenye usajili nchini.


Akiongea leo Alhamisi Mei 29,2025 na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea chuo hicho pamoja na  kuongea na madereva na makondakta wanaochukua mafunzo  katika chuo hicho cha Ufundi Arusha, alisisitiza  elimu wanayoipata itoe matokeo chanya na kuboresha sekta ya usafiri nchini ili kupunguza wimbi la ajali linalotokana na asilimia kubwa ya madereva kutosoma

"Nimewasihi madereva kuhakikisha wanachukua mafunzo ya udereva katika chuo hiki cha Ufundi Arusha pamoja na vyuo vingine vilivyosajiliwa hii itasaidia madereva wetu kuwa na weledi na hivyo kupunguza kama sio kuondoa kabisa wimbi la ajali nchini"

Aidha kamanda Mkonda alisema kuwa jeshi la polisi linaendesha ukaguzi maalumu katika shule za udereva nchini ili kubaini huduma zinazotolewa iwapo kama zinakidhi huduma ya kuzalisha madereva bora.

"Kuna shule kadhaa kwenye ukaguzi wetu tumezifungia na kuwataka wamiliki kufanya mabadiliko na marekebisho yaliyoainishwa lengo ni kuhakikisha zao la darasa lake linakuwa na afya kwa madereva wetu"

"Ninawapongeza sana chuo chetu cha ufundi Arusha kwa hatua hii ya kutoa mafunzo ya uhakika ila ninawasihi mhame kwenye mafunzo ya kawaida na mjikite zaidi kwenye mifumo ya kisasa na kujiimarisha zaidi kwenye teknolojia ya kisasa kujua dunia inaenda wapi"

Aidha alisisitiza kwa chuo hicho kusimamia mafunzo ya kina kwa walimu wa madereva ili kupata walimu waliopikwa na kubobea ili kuwa na uhakika na zao la darasa lake lina kuwa na afya kwa madereva barabarani.

Katika hatua nyingine alisema mifumo ya utoaji leseni imebadilika,  inahitaji ili ubadilishe leseni lazime mhusika ahudhudhulia mafunzo na kudahiliwa 

Awali mkufunzi wa udereva ATC na mkuu wa idara ya uhandisi wa Magari ,mhandisi David Mtongoja alisema mafunzo yanayotolewa kwa madereva chuoni hapo ni ngazi ya diploma na degree.


Alisema chuo cha ufundi Arusha kimeimarishwa kwa miundo mbinu bora ya utoaji wa mafunzo ya udereva ili kufikia malengo ya serikali ya kutokokeza jinamizi la ajili hapa nchini.

Aliwasihi madereva kutumia fursa hiyo kuchukua kozi fupi chuoni hapo kuja kujifunza ambayo itawasaidia kuimarisha sekta ya udereva na kuepusha ajali nchini.





Ends..







Post a Comment

0 Comments