MAPIGANO,WANANCHI WA MONDULI NA LONGIDO WAZICHAPA KUGOMBEA MIPAKA,KADHAA WAJERUHIWA ,LAIGWANANI WAITWA KUPATA SULUHU MKUTANO WA SULUHU UNAFANYIKA LEO

Na Joseph Ngilisho-ARUSHA

WATU kadhaa wanahofiwa kujeruhiwa katika mapigano makali ya kugombea mipaka  baina ya wananchi wa wilaya ya Monduli na Longido Mkoani Arusha .


Mapigano hayo yalizuka juzi katika kijiji cha Nandaare  kata ya Iloryenito wilayani Longido na wananchi wa kijiji cha Rerenden kata ya Engaruka wilayani Monduli.

Akizungumzia tukio hilo diwani wa kata ya Iloryenito,Sanoo Mollel alisema kuwa wananchi Kutoka Monduli walijikusanya na kuvamia upande wa Longido na kupasua tenki la Maji wakilalamikia bikoni za mipaka zilizowekwa wakidai zimemega eneo lao la Monduli.

"Wananchi baada ya kukuta bikoni zimewekwa walipandwa  na jazba  na kujikusanya na kuvamia eneo hilo na kuanza kutoboa na kupasua tenki la Maji wakitumia mikuki wakidai bikoni zilizowekwa zimeingilia eneo lao"Alisema Diwani.

Adha aliongeza kuwa hali hiyo iliwalazimu polisi kufika eneo la tukio na kuanza kufyatua mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya wananchi hao waliokuwa na silaha za jadi zikiwemo fimbo mawe na mikuki.

Kwa mujibu wa diwani huyo,mkuu wa wilaya ya Monduli alifika eneo la tukio na kuwasihi wananchi hao kuacha mapigano wakati serikali inashughulikia mgogoro huo.

Hata hivyo alisema mkuu huyo wa wilaya ya Monduli aliagiza viongozi wa mila Laigwanani kuingilia mgogoro huo ili kuoata suluhu ya kudumu 

Mbunge wa Longido,dkt Steven Kiruswa alipoulizwa alithibitisha kutokea kwa mapigano hayo na kueleza kuwa amelazimika kukatisha safari yake ya kuelekea dodoma na kurejea jimboni kwake ili kushughulikia jambo hilo.

"Mimi ndo naelekea huko na kesho(Leo)mei 16, kuna mkutano na wananchi wa pande zote katika kijiji hicho cha Nandaare na mkutano ukimalizika tutazungumza ila kwa sasa itoshe kwamba tukio hilo lipo  ila siwezi kuongea chochote  maana sijafika eneo la tukio"

Jitihada za kumpata kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo ili kuzungumzia tukio hilo zinaendelea baada ya kutopatikana kupotia simu yake kutopokelewa.

Picha kwa hisani ya Mtandao
.

Ends...




Post a Comment

0 Comments