CRDB YAVIPATIA MAFUNZO NA ELIMU YA FEDHA VIKUNDI 130 VYA UJASIRIAMALI ARUSHA,YATAMBA KUTOA MIKOPO MWEZESHI YA BILIONI 20.2

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

BENKI ya CRDB kupitia Programu ya Imbeju ,imetoa mtaji wa mkopo wezeshi wa sh,bilioni 20.25 kwa vikundi vya ujasiriamali vya wanawake , vijana na makundi maalumu vipatavyo 10,500 tangu mwaka 2023 na kuwapati elimu ya fedha na mafunzo kwa watu wapatao milioni 1.


Aidha katika kipindi cha robo mwaka kutoka Januari hadi Machi Mwaka huu 2025 ,benki hiyo imeshatoa Mkopo wa zaidi ya bilioni 5.6 kwa vikundi mbalimbali nchini.

Hadi kufikia mwisho wa mwezi Machi 2025 tangu mwaka 2023, CRDB Benki imeweza kutoa mikopo yenye thamani ya sh, Trilioni 10.946 kwa sekta zote ,huku zaidi ya asilimia 30 ya mikopo iliwekezwa kwa wajasiriamali wa awali na kati .

Hayo yamebainishwa na afisa Mkuu wa biashara wa CRDB,Boma Rabala wakati wa ufunguzi wa semina ya vikundi vya ujasiriamali zaidi ya 130 vinavyowezeshwa na benki hiyo kutoka wilaya za Arusha ,Longido,Monduli, Arumeru na Karatu Mkoani Arusha.

Rabala alisema kuwa benki hiyo imejipanga kufanya kazi na wajasiriamali kupitia taasisi yake tanzu ya CRDB Foundation kuhakikisha inawafikia watu wenye biashara changa ili waweze kuwa kichocheo cha kukuza uchumi baada ya kupata elimu ya fedha.


"Licha ya jitihada kubwa za uwezeshaji zilizofanyika kuyafikia makundi ya wanawake ,vijana na makundi maalumu, bado uhitaji ni mkubwa hivyo kupitia program ya Imbeju benki yetu imejipanga kuyafikia makundi hayo muhimu kupitia uwezeshaji wa mikopo yenye riba unafuu" 

Alisema kuwa benki hiyo imekuwa ukiendesha bunifu  kwa kushirikiana na serikali kuunga mkono sera ya serikali ya  kutoa mikopo wezeshi ya asilimia 10 kwa makundi maalumu,wanawake na vijana  ili kuwafikia  kwa riba nafuu. 

Alisisitiza kwa wajasiriamali kujiunga kwenye vikundi ili kupata mkopo wezeshi bila kuwa na masharti magumu ikiwemo kuweka dhamana mali isiyohamishika.

Akifungua semina hiyo mkuu wa wilaya ya Arusha Joseph  Mkude aliishukuru benki hiyo kwa ubunifu wa kutoa elimu na mafunzo kwa makundi ya wanawake na vijana ili kunufaika na mikopo wezeshi ya fedha inayotolewa na benki hiyo. Alisisitiza kuwa elimu ya fedha ni nnyenzo   muhimu ya kukuza na kujiimarisha kiuchumi .

"Itumieni semina hii kujiimarisha kiuchumi ili mikopo inayotolewa na benki ya crdb iwanufaishe kiuchumi na taifa kwa ujumla"

Mmoja ya washiriki wa semina  hiyo,Zamaradi Kuwe kutoka Sakina Arusha,aliipongeza benki hiyo kupitia programunya Imbeju kwa kuwapatia elimu na mafunzo ambayo yamesaidia kuwaimarisha kibiashara na kuweza kurejesha mikopo yao bila wasiwasi.

Alisema kikundi chao walichukua mkopo wa Imbeju  na umewasaidia sana,wameweza kurejesha vizuri tofauti na mwanzo walikuwa wakichukua mkopo wa kausha damu, Matone na Tiririka ambayo iliwatesa sana.

"Awali tulikuwa hatuijui mikopo ya Imbeju maana zamani tulikuwa tunachukua mkopo kutoka kausha damu ,Matone na Tiririka ambayo marejesho yake ni kila siku kwakweli iimetutesa sana,tofauti na mkopo wa Imbeju tunalipa kila wiki ama mwisho wa mwezi kwa raha zetu "Alisema.






Ends....











Post a Comment

0 Comments