Na Joseph Ngilisho-ARUSHA
MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Arusha(AUWSA),Mhandisi Justine Lujomba amesema kuwa hali ya upatikanaji wa maji katika jiji la Arusha umefikia kiasi cha asilimia 99 kutoka asilimia 44.
Hatua hii imekuja mara baada ya kukamilika kwa mradi Mkubwa wa kuboresha huduma ya Maji katika jiji la Arusha wenye thamani ya sh,bilioni 520 ambao umeweza kuzalisha kiasi cha zaidi ya lita milioni 200 huku mahitaji yakiwa ni lita milioni 139.
Akiongea mbele ya naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko wakati waziri huyo alipotembelea kituo cha kusukuma maji cha Chekereni wilayani Arumeru ,Mhandisi Lujomba alisema kuwa kabla ya mradi huo jiji la Arusha lilizalisha lita milioni 44 tu na hivyo kushindwa kukidhi mahitaji ya wakazi wake.
"Mradi huu baada ya kukamilika tumepata maji ya ziada tofauti na mahitaji na kupelekea kuhudumia maeneo ya jirani na tunavyoonge muda huu mkandarasi yupo site anapeleka maji eneo la Nanja ambalo haijawahi kupata maji safi na salama,pia kupitia mradi huu tumepeleka maji Mererani"
Alisema utekelezaji wa mradi huo ulihusisha uchimbani wa visima virefu 56 ujenzi wa mabwawa 18 eneo la Terat yenye uwezo wa kutibu maji lita milioni 22 kwa siku ,ujenzi wa mtambo wa kutibu maji upanuzi wa mtandao wa maji taka pembezoni mwa jiji la Arusha wenye urefu wa kilometa 192.
Ujenzi wa vyoo 42 vyenye matundu 184 kwenye maeneo ya shule na masoko,ujenzi wa ofisi kuu tatu za kanda ili kusogeza huduma karibu kwa wananchi,uoanuzi mkubwa wa mtandao wa maji safi katika jiji la Arusha wenye urefu wa kilometa zipatazo 680.
Alisema ujenzi wa vituo 18 vya maji ya zima moto kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya moto.
Mhandisi Lujomba alizitaja faida mbalimbali baada ya kukamilika kwa mradi huo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa uwezo wa kuzalisha maji kutoka wastani wa lita milioni 40 hadi kufikia lita milioni 200,kuongezeka kwa wigo wa matandao wa maji taka kutoka asilimia 7.6 hadi kufikia asilimia 39.5 katikati ya jiji la Arusha.
Pia alisema wateja wameongezeka kutoka wateja 80,037 hadi kufikia wateja 133,847 hadi disemba 2024,pia wateja walioungwa kwenye mfumo wa maji taka wameongezeka kutoka wateja 3300 hadi wateja 10,856 hadi disemba 2024.
Wakandarasi waliotekeleza mradi huo waliweza kununua bidhaa katika soko la ndani vyanye thamani ya sh,bilioni 150 hivyo kuchangia pato la taifa pia mradi umesaidia upatatikanaji wa ajira ambapo wastani wa watu 15,000 walinufaika na mradi huo.
Pia mradi huo umenufaisha wananchi wapatao 1072 kwa kuwalipa fidia kiasi cha sh, bilioni 6.08,ujenzi wa mtandao wa umeme umewanufaisha wananchi ambao hawakuwahi kupata huduma hiyo.
Ends....
0 Comments