WAZIRI BITEKO ATUA HOSPITALI YA MERU AWAHAKIKISHIA WANANCHI UWEKEZAJI MKUBWA SEKTA YA AFYA,APONGEZA MRADI WA MAJENGO!

 SERIKALI KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA AFYA - DKT. BITEKO 

By Arusha digital.com


Serikali imeahidi kuendelea kuboresha huduma za Afya nchini katika ngazi zote ili kuboresha huduma za Afya kwa Watanzania. 


Hayo yamesemwa Aprili, 25, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Dkt. Doto Biteko akiwa ziarani Mkoani Arusha ambapo amesema kuwa lengo la uwekezaji katika sekta ya afya ni kusigeza huduma za afya kwa wananchi." 


Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea na uwekezaji mkubwa unaofanya kwa kujenga hospitali, vituo vya afya na zahanati katika maeneo mbalimbali nchini. 







Akizungumza baada kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Meru, iliyopo Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha, Mhe. Dkt. Biteko alisema lengo la uwekezaji katika sekta ya afya ni kuboresha afya za Watanzania. 


“ Kama mnavyofahamu afya ndio mtaji wa wananchi na Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali mpya na kufanyia ukarabati zilizopo,” Alisema Dkt. Biteko. 


Alisistiza “ Watu wote nilioongea nao hapa hospitalini wamesema hali ya utoaji huduma imeimarika na ni nzuri, nataka niwaambie Rais Samia katika uongozi wake ameapa kuboresha hali za maisha ya Watanzania.


 Hapo awali ilimlazimu mgonjwa kutoa makohozi siku tatu mfululizo ili kumfanyia kipimo cha ugonjwa wa kifua kikuu, leo tuna mashine ya kisasa inayotumia saa mbili kupata majibu ya mgonjwa,” 


Alisema ujenzi  na maboresho yaliyofanyika hospitalini hapo  imetumia raslimali za ndani (force account) na kazi imefanyika kwa ubora na kuzingatia thamani ya fedha. 


Aliongeza kuwa katika kuelekea miaka 61 ya Muungano uwepo wa hospitali hiyo ni kiashiria cha kuwa nchi inapiga hatua kimaendeleo. Hivyo, wananchi hawana budi kuuenzi na kuutunza Muungano. 


Aidha, amewataka wagonjwa kuwa wavumilivu wanapoenda kupata matibabu huku wakizingatia kuwa wahudumu wa afya wanafanya jitihada kubwa kuwapa huduma bora. 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda alisema kuwa wananchi wa eneo hilo wanafurahia huduma nzuri zinazotolewa na sasa idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa ni 12,000 kutoka 3,000 ya awali.

  




Ends..

Post a Comment

0 Comments