MAKONDA AMCHAPA ZA USO GAMBO MBELE YA WAZIRI BITEKO ,ADAI AMEUMIZA SANA WATU ,AMTAKA AOMBE RADHI HADHARANI WOTE ALIOWAUMIZA ,

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda ,amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo kuwaomba radhi hadharani watu wote aliowaumiza kwa kuwafitini na kuwachonganisha na kuwazushia uongo .


Makonda alimpongeza Gambo kwa kuomba radhi katika jaribio lake la kutaka kupenyesha uongo katika bunge la Tanzania kwa kutuhumu ufisadi katika jengo la utawala la jiji la Arusha pamoja na kumtuhumu uongo waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa.

Makonda ametoa kauli hiyo kali mbele ya Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati Dr  Doto Biteko huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wamefurika katika viwanja vya Kilombero jijini Arusha.


Makonda alisema kuwa Gambo ameumiza watu sana wakiwemo viongozi wasio na hatia na kwamba iwapo uongo wake wa kugawa fitina Bungeni  ungepita viongozi  wengi wangepoteza kazi lakini bunge lilikuwa makini na kubanini uongo huo uliomlazimu kuomba radhi kabla ya kusulubiwa na kamati ya maadili ya bunge.


“Nampongeza kwa sababu moja kubwa, juzi ameomba radhi bungeni, amechonganisha chonganisha sana watu hapa na leo hapa ameanza kumsifia DC wangu (Mkuu wa Wilaya) kwa sifa zilezile ambazo alinisifiaga mimi nilipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa"

"Lakini sasa hivi hata kulitamka jina la Makonda hawezi, namsifu kwa sababu aliomba radhi. Alikuwa anaenda kuharibu maisha ya watu kwa kuwadanganya wabunge na kama Bunge lisingekuwa makini na Waziri wetu Mchengerwa kuwa imara, leo hii kuna watu wangepoteza kazi" amesema Makonda.

Makonda amesisitiza kuwa, bila Gambo kuwaomba radhi watu aliowaumiza, hatopata kibali mbele ya Mungu na wanadamu.

“Mambo yalivyoendelea yalipelekea simu ninazopata, unamuita Waziri wetu muongo. Hii stendi inayoanza kujengwa, hii nimemuomba Mchengerwa. Ilikuwa dizaini ndogo haikidhi viwango, akaongeza bajeti bilioni 30 ni faida kwa wananchi wa jiji, halafu unamuita Waziri wetu muongo".

"Kwa kuwa Bunge limemsamehe, mimi moyoni sina shaka naye, lakini sharti langu moja aliowaumiza na kuharibu maisha yao awaombe radhi, ili mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu tupate kibali cha kuifanya kazi hii".

Ends..


Post a Comment

0 Comments