Kigogo huyo amekuwa akiwaita wagombea na wapiga Kura ofisini kwake na kuwapa Maelekezo juu ya Viongozi wa juu kumtaka Mgombea huyo hali inayoleta sitofahamu Kwa Baadhi ya Wagombea na kuhatarisha Amani na vurugu ndani ya Chama Arusha.
Kwa Mujibu wa Vyanzo vya habari ndani ya chama vimedai kuingiliwa Kwa Uchaguzi na Viongozi wa Serikali ni kosa Kwa Mujibu wa Kanuni ndani ya Chama na Kudai ni Maelekezo ya Juu ni Kuwadanganya wana CCM na wana CCM Arusha wameomba Kigogo kukaa pembeni ili vikao vya juu vya Chama vitoe maamuzi yenye kukijenga chama Mkoa wa Arusha na sio vinginevyo.
Kwa mujibu wa chanzo muhimu ndani ya chama hicho kikongwe,baadhi ya wafuasi wa chama hicho wanajipanga kupiga kura ya turufu ,kutokuwa na imani na kigogo huyo katika afya ya siasa mkoani hapa wakitaka mwajiri wake amwondoe.
Mwisho
إرسال تعليق