EALA WATAKA VISA YA PAMOJA KWA MASHABIKI WA AFCON 2027
Na Joseph Ngilisho | ARUSHA
Kadaga alisema utaratibu huo unalenga kuwawezesha mashabiki kuvuka mipaka ya nchi hizo tatu kwa urahisi zaidi kufuatilia mechi za mashindano hayo yatakayofanyika kwa ushirikiano wa mataifa hayo.
Alitoa kauli hiyo wakati wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), wakiongozwa na Spika wake, Joseph Ntakirutimana, walipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Pamoja AFCON jijini Arusha, Oktoba 11, 2026.Alisema ushirikiano wa nchi hizo katika maandalizi ya mashindano hayo ni muhimu katika kuhakikisha yanafanyika kwa mafanikio, huku akipongeza Serikali ya Tanzania na timu ya wahandisi kwa uwekezaji katika miundombinu ya michezo.
Ujenzi wa Uwanja wa Pamoja AFCON umefikia asilimia 95, huku kituo hicho kikiwa miongoni mwa miradi muhimu inayolenga kuwezesha Tanzania kutekeleza wajibu wake wa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya mwaka 2027 kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.
Maandalizi hayo yanaendelea sambamba na maandalizi ya Arusha kuwa mwenyeji wa Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki itakayofanyika Desemba 4 hadi 16, 2026.
Michezo hiyo inatarajiwa kuwakutanisha wabunge kutoka mabunge ya nchi zote nane wanachama wa EAC, kwa lengo la kuimarisha umoja, ushirikiano na utangamano wa kikanda.
Ziara ya ukaguzi wa uwanja huo iliandaliwa na kuratibiwa na EALA ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya kufuatilia miradi ya EAC na kushirikiana na wadau katika kuendeleza maendeleo ya kikanda.
Ends




Post a Comment