TANROADS YAANZA MAANDALIZI KUKABILI EL NINO ARUSHA
Na Joseph Ngilisho | ARUSHA
Hatua hiyo inalenga kubaini maeneo hatarishi na kuyafanyia kazi kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua unaotarajiwa kuanzia Oktoba mwaka huu.
“Ukaguzi huu wa barabara unakuja pale ambapo TANROADS inaendelea kujiandaa na mvua za El Niño ambazo zinatarajiwa kunyesha kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu,” alisema.
Alisema maandalizi hayo yanafanyika mapema ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa mvua, badala ya kusubiri mvua zianze ndipo hatua zichukuliwe.
“Hatua hizi zinachukuliwa mapema, lengo si kusubiri mvua zinaponyesha ndipo tatizo litokee, bali ni kutambua maeneo hatarishi mapema na kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha barabara inaendelea kuwa salama na kupitika,” alisema.
Alisema mtaro huo utasaidia kuelekeza maji ya mafuriko yanayotoka katika maeneo ya milimani ya Meru kwenda Mto Maji ya Chai, hatua inayolenga kupunguza athari za mafuriko katika maeneo ya wananchi.
Alisema sambamba na ujenzi wa mtaro huo, inajengwa pia barabara ya mchepuko (service road), ambayo itasaidia kuimarisha usalama wa wananchi na kupunguza madhara yanayotokana na maji ya mafuriko.
Hatua hiyo imepokelewa na baadhi ya wakazi wa Jiji la Arusha wanaokabiliwa na changamoto ya maji na mafuriko wakati wa mvua.
Mkazi wa Jiji la Arusha, Joseph Mgaiwa, alisema kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya maji na mafuriko, hivyo kupongeza ujenzi wa mtaro huo akisema unaweza kuwa suluhisho la kudumu kwa tatizo hilo.
Eda Msavange, ambaye ni mkazi wa Jiji hilo, alisema wananchi wamekuwa wakipata adha ya maji machafu wakati wa mvua, hivyo kueleza matumaini kuwa ujenzi wa mtaro huo utaleta nafuu na kuongeza usalama.
Mhandisi Massawe alisema kazi za maandalizi ya msimu wa mvua hazijaishia katika Barabara ya Arusha–Moshi pekee, bali zinaendelea pia katika barabara za Arusha–Namanga na Arusha–Minjingu.
Alisema katika maeneo hayo, TANROADS inaendelea na kazi za kuzibua mitaro na madaraja ili kuhakikisha maji yanapata njia sahihi ya kupita na kupunguza uwezekano wa kusababisha uharibifu wa miundombinu.
Naye Msimamizi wa Mradi kutoka Kampuni ya Rocktronick Limited, Godfrey Mushi, alisema kampuni hiyo itahakikisha kazi za mradi huo zinakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.
Alisema lengo ni kuhakikisha miundombinu hiyo inakuwa tayari kabla ya kuanza kwa mvua za El Niño.
Ends










Post a Comment