MBUNGE GIDO AWAKUMBUKA VIJANA WA UVCCM, AKABIDHI MSAADA WA VYAKULA
Na Joseph Ngilisho | ARUSHA
Msaada huo umekabidhiwa leo, Septemba 30, 2026, kwa niaba ya Mbunge huyo na Msaidizi wake, Lairumbe Laizer, aliyemkabidhi mifuko ya vyakula Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha Mjini, Hassan Mndeme.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Laizer alisema msaada huo ni sehemu ya juhudi za Mbunge Gido kuhakikisha vijana wanaoshiriki katika shughuli za chama wanapata mazingira yanayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Alisema Mbunge Gido anatambua nafasi kubwa ya vijana katika kujenga chama na taifa, hivyo ataendelea kushirikiana nao na kuunga mkono jitihada zinazolenga kuwaandaa kuwa viongozi na watendaji bora wa sasa na wa baadaye.
“Mhe. Marirta Gido anaamini vijana ni nguvu kazi na msingi muhimu wa maendeleo ya taifa. Ndiyo maana ameona umuhimu wa kuunga mkono kambi hii kwa kuhakikisha vijana wanapata mahitaji muhimu wakati wakiendelea na mafunzo yao,” alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha Mjini, Hassan Mndeme, amemshukuru Mbunge Gido kwa kutambua mahitaji ya vijana na kuonesha utayari wa kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali za chama.
Mndeme alisema msaada huo umefika wakati muafaka na utasaidia kupunguza changamoto za mahitaji ya chakula kwa vijana wanaoshiriki katika kambi hiyo.
Hatua hiyo inaendelea kuimarisha uhusiano wa karibu kati ya Mbunge Gido na vijana wa UVCCM, huku ikionesha namna viongozi wanavyoweza kutumia nafasi zao kuunga mkono shughuli za chama na kuwajengea vijana mazingira bora ya kujifunza, kushiriki na kutekeleza majukumu yao.
Ends..



Post a Comment