Na Joseph Ngilisho- Arushadigital
Bei ya mafuta ya petroli imepanda kwa kiwango kikubwa katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo sasa lita moja inauzwa kwa shilingi 3,820 mwezi Aprili 2026, kutoka shilingi 2,864 mwezi Machi. Ongezeko hilo limetangazwa rasmi na Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) katika taarifa yake ya marekebisho ya bei za mafuta.
Kwa mujibu wa EWURA, kupanda kwa bei kunachangiwa na mabadiliko katika soko la kimataifa, ikiwemo ongezeko la bei ya mafuta ghafi pamoja na changamoto za usafirishaji. Aidha, hali ya kisiasa na kiusalama duniani imeendelea kuathiri upatikanaji na usambazaji wa mafuta, jambo linalosababisha gharama kupanda katika masoko mbalimbali.
Mamlaka hiyo imeeleza kuwa gharama za uagizaji zimeongezeka kutokana na kupanda kwa bei za bima ya meli, ucheleweshaji wa mizigo na gharama za usafirishaji kwa ujumla. Bei hizo mpya zimeanza kutumika rasmi kuanzia Aprili Mosi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.





0 Comments