By Arushadigital-Dar Es Salaam
Wakati kukiwa na sintofahamu ya ukweli wa alipo Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO), Faustine Mafwele na kile kinachozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii, Kamanda wa kanda hiyo, Jumanne Muliro ametoa kauli.
Hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii, watu waliodai kuliwakilisha kundi linalojiita Tanganyika Freedom Fighters (TFF) walichapisha ujumbe unaomuhusisha Mafwele, katika madai mbalimbali ambayo hayajathibitishwa rasmi.
Katika ujumbe huo, watu hao walitoa kauli kali dhidi ya Mafwele wakimtuhumu kwa masuala yanayohusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Akifafanua sintofahamu hiyo, Kamanda Muliro ameufananisha ujumbe wa kundi hilo kama riwaya za Shabaan Robert za kusadikika.
Amesema katika mambo ya kusadikika unaweza kusikia mtu amekufa halafu ukamuona.
Kamanda Muliro ametoa kauli hiyo alipoulizwa swali na mwandishi wa Mwananchi kuhusu ukweli wa ujumbe wa kundi hilo na alipo ZCO Mafwele.

0 Comments