By Arushadigital
Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Raila Odinga amefariki dunia katika Wilaya ya Kerala Nchini India akiwa na umri wa miaka 80 baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati akiwa anafanya mazoezi katika matembezi ya asubuhi.
Vyombo vya Habari Nchini Kenya na India vimeripoti kuwa Odinga alikuwa Nchini India kwa matibabu kwa zaidi ya siku tano sasa na alipata shambulizi la moyo kufeli ghafla akiwa ameambatana na Mtoto wake wa kike na Dada yake.
Raila Odinga alizaliwa January 7, 1945 na alikuwa Waziri Mkuu wa Kenya kutoka mwaka wa 2008 hadi 2013 lakini pia amewahi kuwa Mgombea Urais nchini humo aliyeungwa mkono na Wafuasi wengi.
Kabla ya kuwa Waziri Mkuu alikuwa Mbunge wa Langata kuanzia 1992 hadi 2007 kisha akahudumu kwenye Baraza la Mawaziri la Kenya kama Waziri wa Nishati kuanzia 2001 hadi 2002 na baadaye kama Waziri wa Barabara, kazi ya umma na makazi kuanzia 2003 hadi 2005 na kisha akateuliwa kuwa Mwakilishi wa juu wa maendeleo ya miundombinu katika Umoja wa Afrika mwaka wa 2018.

0 Comments