CCM YATANGAZA VIKAO VYA MCHUJO WA WAGOMBEA UBUNGE!

By Arushadigital -DODOMA 


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza ratiba ya vikao vyake vya kitaifa, vitakavyofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais Samia Suluhu Hassan.


Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitapewa nafasi ya kwanza na kitafanyika tarehe 21 Agosti 2025. Baada ya hapo, Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kitafanyika tarehe 23 Agosti 2025.


Ajenda kuu ya vikao hivyo ni kufanya uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwemo: Wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Viti Maalum, pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Viti Maalum vya Baraza la Wawakilishi.

Post a Comment

0 Comments