Arushadigtal -Ahmedabad, India
Ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Air India imeanguka na kuwaka moto leo Juni 12, 2025, muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Ahmedabad, India, kuelekea London, Uingereza.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini India, ndege hiyo aina ya Boeing 787-8 Dreamliner yenye usajili namba VT-ANB na serial namba 36279, ilikuwa na jumla ya watu 242 ndani yake. Kati yao, 230 walikuwa abiria na 12 walikuwa wafanyakazi wa ndege.
Tukio hilo limetokea ghafla baada ya ndege kupaa, ambapo iliripotiwa kupoteza mawasiliano na kituo cha udhibiti wa anga kabla ya kuanguka na kushika moto katika maeneo ya karibu na uwanja wa ndege.
Vikosi vya dharura na zimamoto viliwasili kwa haraka eneo la tukio na kuanza juhudi za uokoaji. Hadi sasa, juhudi hizo bado zinaendelea huku idadi kamili ya majeruhi au waliopoteza maisha haijathibitishwa rasmi. Serikali ya India imethibitisha kuwa uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo umeanzishwa na wataalamu wa usalama wa anga.
0 Comments