Na Joseph Ngilisho-ARUSHA
MKUU wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ametembelea maonesho ya Karibu Kilifair na kufanya ukaguzi wa Mwisho katika Viwanja vya Magereza yanayotarajiwa kufunguliwa kesho na naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati Dotto Biteko.
Akizungumza leo June 5,2025 na Vyombo vya Habari baada ya kutembelea, Makonda amesema maandalizi yamekamilika kwa Asilimia kubwa na kuwakaribisha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Maonyesho hayo ya kitalii na kuchangamkia Fursa mbali mbali katika kukuza uchumi wa taifa na kujiongezea kipato .
"Maonesho haya yanayotarajiwa kufunguliwa kesho ni tukio la aina yake tulipoanza matangazo haya tulikuwa na nchi Takribani 40 lakini hadi leo ikiwa imebaki siku moja tuna nchi 52 na makampuni zaidi ya 500 yanashiriki maonesho hayo"
0 Comments