IGP WAMBURA APANGUA MA- RPC AMFYATUA KATABAZI DODOMA,RPC ARUSHA YUPOYUPO SANA

 By arushadigtal


Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillus Wambura, amepangua makamanda watatu, akiwamo RPC wa Dodoma.


Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi leo Juni 17, 2025 imeeleza kuwa  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), George Katabazi ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Dodoma.


 Imesema nafasi yake imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Galus Hyera, ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli.


"Aidha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Matride Kuyeto, amehamishwa kutoka Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli.

"Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayofanyika ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi," imefafanua taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments