HAYA HAPA MAJIMBO YA UCHAGUZI YALIYOGAWANYWA NA TUME YA UCHAGUZI,TAZAMA JIMBO LAKO HAPA

By arushadigtal-DODOMA

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuanzishwa kwa majimbo mapya nane ya uchaguzi pamoja na kubadilishwa kwa majina ya majimbo mengine 12, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.



Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Tume hiyo,Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele, amesema uamuzi huo umezingatia ongezeko la watu, ukubwa wa maeneo ya kiutawala, pamoja na mahitaji ya uwakilishi wa karibu zaidi kati ya wananchi na wawakilishi wao bungeni.


Kwa mujibu wa Jaji Mwambengele, majimbo mapya yaliyoundwa ni kama ifuatavyo:


πŸ“ŒDar es Salaam:

Jimbo la Ukonga limegawanywa na kuanzishwa Jimbo la Kivule

Jimbo la Mbagala limegawanywa na kuanzishwa Jimbo la Chamazi



πŸ“ŒMbeya:

Jimbo la Mbeya Mjini limegawanywa na kuundwa Jimbo la Uyole



πŸ“ŒDodoma:

Jimbo la Dodoma Mjini limegawanywa na kuundwa Jimbo la Mtumba



πŸ“ŒSimiyu:

Jimbo la Bariadi limegawanywa na kuundwa Jimbo la Bariadi Mjini



πŸ“ŒGeita:

Jimbo la Busanda limegawanywa na kuanzishwa Jimbo la Katoro

Jimbo la Chato limegawanywa na kuundwa Jimbo la Chato Kusini



πŸ“ŒShinyanga:

Jimbo la Solwa limegawanywa na kuanzishwa Jimbo la Itwangi



Aidha, Tume hiyo imesema majina ya majimbo 12 ya uchaguzi yatafanyiwa mabadiliko ili kuendana na mabadiliko ya kiutawala, kijografia na mahitaji ya kitaifa ya utawala bora. Orodha kamili ya majimbo yaliyoathiriwa na mabadiliko ya majina inatarajiwa kutangazwa rasmi katika tangazo la serikali litakalotolewa hivi karibuni.



Tume imewahakikishia Watanzania kuwa mchakato huo umezingatia misingi ya usawa, haki na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali, na unalenga kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka huu unafanyika kwa uwazi, haki na kwa kuzingatia uwakilishi wa kweli wa wananchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post