DIWANI AJIVUNIA UTEKELEZAJI MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO KATANI KWAKE

 DIWANI WA KYAITOKE AJIVUNIA UTEKELEZAJI MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO KATANI KWAKE


Na Lydia Lugakila

Bukoba


Diwani wa kata ya Kyaitoke Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Mhe, Seveline Kaijage Kijoma ameeleza miradi mikubwa ya maendeleo ambayo imetekelezwa katika kata yake ya Kyaitoke kupitia mkono wake pamoja na Serikali, Mbunge wa Jimbo la Bukoba vijijini Dkt. Jasson Rweikiza, wahisani wananchi.


Akieleza kupitia taarifa yake wakati akizungumza na Malunde 1 blog iliyotaka kujua ni miradi ya maendeleo iliyofanyika kata hiyo kwa kipindi cha mwaka 2021 Hadi 2025 Kijoma amesema kuwa kwanza anaipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio makubwa ya miradi ya maendeleo ilipatikana.


Akielezea utekelezaji wa miradi mikubwa iliyofanyika upande wa Elimu Diwani huyo amesema wamefanikiwa katika ujenzi wa vyumba madarasa tisa shule ya Sekondari Izimbya, ujenzi wa maabara moja shule ya Sekondari Izimbya, ujenzi wa matundu kumi ya vyoo vya wasichana shule ya Sekondari Izimbya, ofisi mbili za walimu shule ya Sekondari Izimbya, msaada wa madawati 140 shule za msingi Kyaitoke na Kikagati toka Bank ya NMB, kulipa posho za Walimu wa kujitolea shule za msingi na Sekondari, kuhakikisha na kusimamia lishe shuleni,  kupiga vita na kupambana na suala la utoro na mimba za utotoni kwa shule za msingi na Sekondari kata Kyaitoke.


Kijoma akifafanua yaliyofanyika katika upande wa Afya amesema wamefanikiwa katika kusimamia na kuhakikisha watoto wote  wanakwenda kliniki ikiwa ni pamoja na akina mama wajawazito, kuhamasisha na kuhakikisha watoto wanapata lishe bora, kusimamia vyema zoezi la usafi na utunzaji wa mazingira, ujenzi wa kliniki ya akina mama na mtoto Kabwenge ambapo msingi umekamilika.


"Katika upande wa huduma ya maji tumefunga mashine pamp za maji mpya 10 kijiji Kyaitoke, kusimamia usafi wa mara kwa mara kwa wale wanaotumia madimbwi au mabwawa ya maji, uchimbaji wa visima  vinne virefu vya maji kupitia Ruwasa, Mayawa, Orthodox na uchimbaji wa visima vitatu vifupi vya maji katika kijiji cha Rugaze shirika la waislamu, uchimbaji wa kisima kirefu kimoja cha maji Izimbya Sekondari na kulinda vyanzo vya maji visiharibiwe "amesema Diwani huyo.


Ameongeza kuwa katika upande wa muindombinu ya umeme kwa mwaka 2021 hadi 2025 umeme umesambaa katika vijiji viwili vya Kyaitoke na Rugaze, katika vitongoji umeme umefungwa katika vitongoji sita ambapo vitongoji nane tayari vina umeme.


"Umeme pia umefungwa  na kuwashwa katika shule ya Sekondari Izimbya, shule ya msingi Mwenge, shule ya msingi Igoma, shule ya msingi Rugaze na zahanati ya Rugaze"


Amesema katika upande wa Barabara wamefanikiwa katika ukarabati wa mara kwa mara katika barabara ya kibale, kasikizi na Ruhunga, ujenzi wa makalvati sita mapya barabara ya kabale, kasikizi na Ruhunga, uchimbaji wa mitaro mitatu mikubwa na mirefu ya kupitisha maji yenye urefu wa mita 300.


Aidha katika upande wa kilimo na ufugaji Diwani huyo amepamba na kuhakikisha anahamasisha Wananchi wanakuwa na akiba ya chakula kwa ajili ya familia zao, kutafuta Wataalam wa kilimo waliowatembelea wakulima na wafugaji na kuwapa ushauri pale walipopata changamoto katika shughuli zao, kwa kushitikiana na Wananchi wamedhibiti wanyama waharibifu wa mazao ya Wananchi wakiwemo Tembo, Ngedere, Nguruwe katika vijijini vya Kyaitoke na Rugaze.


Ameongeza kuwa katika suala la ulinzi na usalama amefanikiwa kudhibiti wizi mkubwa uliokuwepo kwenye mali za Wananchi ambapo ameshirikiana na watendaji wa Serikali vijiji na kata, amehakikisha pia anahamasisha wenyeviti wa vijiji na vitongoji kufanya vikao na mikutano ya mara kwa mara kwa mujibu wa taratibu na kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi ikiwemo migogoro mbali mbali.


Diwani huyo amesema kuwa anajivunia kukamilisha miradi viporo ikiwa ni pamoja na maabara moja Izimbya Sekondari, kukamilisha ujenzi wa kliniki ya akina mama na mtoto Kabwenge na Rugaze pamoja ukamilishaji miradi mipya kwa mwaka 2025-2026 ambayo ni ujenzi wa chumba kimoja cha darasa shule ya msingi Mwenge ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Rugaze shule ya msingi, ujenzi wa choo matundu 15 Igoma shule ya msingi, kufunga na kusambaza maji vitongoji vyote Kyaitoke na Rugaze kupitia Ruwasa, kufunga na kusambaza umeme vitongoji 3 ukarabati mkubwa Ofisi ya utawala kata Kyaitoke,ujenzi wa shule shikizi Sekondari kata Kyaitoke, ujenzi wa Barabara Ndama kinshuli, Kikagati, ujenzi wa Barabara Izimbya, Omkombo hadi Rugaze(Akabanda)


Hata hivyo Kijoma ametoa shukrani zake kwa chama cha Mapinduzi CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM katani humo Benjamini Mwesiga Rufulenga kwa umakini na kusimamia vizuri kata hiyo jambo lililosababisha viongozi na watendaji wa Serikali wanatekeleza vizuri ilani ya chama hicho 2020-2025, amewashukuru viongozi wa Halmashauri za vijiji Kyaitoke na Rugaze kwa ushirikiano mkubwa na wa karibu, watendaji na watumishi wote wa zamani na wa Sasa waliompa ushauri, pia ameshukuru chama na Serikali Wananchi, viongozi wa vyama wote, viongozi wa dini huku akiwaomba kuendelea kushirikiana na kushauriana ili kuweza kukamilisha viporo vilivyobaki katika kipindi kijacho kwani penye mafanikio hapakosi changamoto.

Post a Comment

0 Comments