ONA BODABODA ARUSHA WANAVYOMPENDA RAIS SAMIA , WAGOMBEA KEKI WAKIMTAKIA HAPPY BATH DAY 'MITANO TENA' WAMSHUKURU KWA KUWAPATIA OFISI YA KISASA

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 



UMOJA wa waendesha Bodaboda Mkoa wa Arusha (UBOJA) wameadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukata keki na kupanda miti katika Ofisi zao zilizoko katikati ya Jiji la Arusha ikuwa ni ishara ya Upendo na kumtakia maisha Mema na marefu zaidi.

Hafla ya sherehe hizo zilizoenda sambamba upandaji Miti, wakisema lengo ni kutambua mchango mkubwa uliofanywa na kiongozi huyo mkubwa hapa nchini.

Mwenyekiti wa UBOJA Constantine Okello alisema baadhi ya mambo makubwa iliyopelekea wao kuadhimisha sikukuu hiyo mbali na kushusha kiwango cha faini kutoka Sh30,000 hadi sh10,000 kwa makosa ya barabarani lakini pia kuwajengea Ofisi ya chama mwaka jana na kuwachangia jumla ya Sh10 milioni za kuanzisha Ushirika wa Umoja wao.
 










Post a Comment

0 Comments